LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 3, 2023

WANUFAIKA WAELEZA WAHARIRI WA HABARI MFUKO "WCF IMETUFUTA MACHOZI"

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WANUFAIKA wa fidia inayotolewa na WCF, wametoa ya ‘moyoni’ mbele ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, kwa kile walichokiita Mfuko huo umewafuta machozi.

Wakitoa ushuhuda Novemba 2, 2023, katika kikao kazi baina ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na Wahariri wa vyombo vya habari, kuelezea utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya Mfuko huo, miaka 8 tangu kuanzishwa kwake.

Beauty Jackson Letema, ni mnufaika wa WCF, yeye ni mama mjane ambaye alifiwa na mumewe katika ajali wakati akitekeleza majukumu ya mwajiri wake.

“Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, lakini pia naishukuru WCF, mume wangu alipofariki aliniacha na watoto watatu na ujauzito, WCF walianza kunihudumia mimi na watoto wangu hao watatu na kisha huyu mwingine, Mimi sikuwa na kazi yoyote ya kufanya, WCF wanatuhudumia mimi na watoto, tunavaa, tunakula na pia watoto wangu wanasoma bila shaka yoyote, kwakweli wamenifuta machozi.” Alisema

Kutokana na manufaa anayoyapata kutoka WCF, Mnufaika huyo aliwahimiza waajiri kujisajili na mfuko ili wafanyakazi wanapopatwa na madhila wakiwa kazini, basi Mfuko utakuwa mfariji wao.

“Wito wangu kwa waajiri, WCF ni mfuko wenye faida sana, kama mimi mume wangu alivyofariki na mwajiri wake angekuwa hajajisajili WCF, maisha yangekuaje?  Natoa wito kwa waajiri wajiunge na WCF.” Alisisitiza Beauty.

Mnufaika mwingine ni Halima Sheikh, wakati akitekelza jukumu lake kama dereva wa bus la abiria, Super Feo, alikatika mkono baada ya bus alilokuwa akiliendesha kupinduka.

“Baada ya kupoteza mkono na kupata ulemavu wa kudumu, WCF imekuwa ikinilipa fidia kila mwezi, malipo yananisaidia mimi na familia yangu, nimeambiwa nitalipwa maisha yangu yote, hakika nafarijika sana.” Alisema.

“Kwa kifupi naishukuru sana Serikali kwa kuanzisha WCF, Mfuko una manufaa makubwa sana, ninajitegeema asilimia 100, namshukuru Mkurugenzi Mkuu wa WCF na timu yake, Mfuko umenipatia matibabu vizuri sana hadi kupona,  maisha yangu yanaendelea.” Alisema Mnufaika mwingine, Bw. Hassan Sima Jambau, aliyekuwa mtumishi wa Televisheni ya Taifa, TBC.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dk. John Mduma akiwasalimia wanufaika wa fidia inayotolewa na WCF, baada ya kikao kazi baina na Wahariri na Mfuko huo kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Beauty Jackson Letema, mnufaika wa WCF, akitoa ushuhuda mbele ya Wahariri wa habari na Waandishi wa habari wakati wa kikao kazi hicho, jana.
Halima Sheikh.

Mzee Joe Nakajumo ambaye ni Mhariri wa Habari wa siku nyingi, akisikiliza kwa maini shuhuda zilizokuwa zikitolewa na wanufaika wa WCF wakati wa kikao kazi hicho.

Mkurugenzi Mkuu wa WCF Dk. John Mduma (kushoto), akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Thobia Makoba wakati wa kikao kazi hicho.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages