Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Chama Cha Wataalam wa Radiografia Tanzania (Tanzania Association of Radiography -TARA), jana Novemba 08, 2023, kilifanya maadhimisho ya kila mwaka ya siku ya huduma ya Radiography (Radiography Day), kwa kutoa mafunzo kwa baadhi ya shule za Sekondari zenye michepuo ya Sanyasi za jijini Dar es Salaam, Njombe na Tabora.
Rais wa TARA Bakari Msongamwanja amesema leo kwamba katika shamrashamra za maadhimisho hayo jana, Wataalamu kutoka chama hicho walitoa mafunzo kwa walimu na wanafunzi wa shule za Jangwani, Azania na Tambaza, katika Ukumbi wa Taasisi ya Mifupa (MOI).
Amesema aliongoza maadhimisho hayo akiwa na viongozi wengine wa TARA wakiwemo Katibu Naibu Mwenyekiti Wilson Ngowi na Katibu Omari Msewa, huku viongozi Aurelia akiendesha mafunzo hayo wa wanafunzi na walimu wa baadhi ya shule mkoani Njombe na Jumanne akiwa katika Shule ya Sekondari Uyuwi mkoani Tabora.
Msongamwanja amesema pamoja na kutoa mafunzo ya Radiographer kwa walimu na wanafunzi katika maadhimisho hayo, mwaka huu TARA inatoa pia huduma za uchunguzi wa afya kwa wananchi kwa kutumia vipimo vya mashine za MRI, CT Scan, Ultrasound na X-ray na pia kufanya matibabu ya Saratani kwa njia ya mashine za mionzi, Linear CT, PET CT na miozi.
Amesema, maadhimisho ya huduma za Radiography hufanyika kila Novemba 8, ambapo duniani kote Wataalam wa uchunguzi tiba huitumia siku hiyo katika kutenda matendo ya huruma, elimu na kujitafakari katika utoaji wa huduma.
Msongamwanja amesema kilele cha maadhimisho ya huduma za Radiografia nchini Tanzania kitafanyika mkoani Mbeya kesho na keshokutwa (Novemba 10-11, 2023) ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Mabunge la Dunia Dk. Tulia Akson.a 10-11/11/2023 huku mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Mabunge la Dunia Dk. Tulia Akson.
Your Ad Spot
Nov 9, 2023
Home
Afya
featured
TARA WAADHIMISHA SIKU YA HUDUMA ZA RADIOGRAFIA KWA KUTOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI SHULE ZA MICHEPUO YA SAYANSI, DAR, NJOMBE NA TABORA
TARA WAADHIMISHA SIKU YA HUDUMA ZA RADIOGRAFIA KWA KUTOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI SHULE ZA MICHEPUO YA SAYANSI, DAR, NJOMBE NA TABORA
Tags
Afya#
featured#
Share This
About CCM Blog
featured
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot










No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇