Na Victor Makinda, Morogoro
Wito umetolewa kwa viongozi wenye tabia ya kutumia vibaya madaraka yao kuwakandamiza na kuwatesa watu wa tabaka la chini, kuacha tabia hiyo kwani sio tu chukizo kwa biniadamu bali pia ni chukizo kwa Mungu.
Wito huo umetolewa mjini Morogoro jana na Askofu Kanisa la Kiinjili, Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Morogoro, Jacob Mameo, wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la la uzinduzi wa siku 16 za kupinga katili wa kijnisia lililoandaliwa na kanisa hilo.
Askofu Mameo alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi katika jamii zetu ambao huyatumia vibaya madaraka yao kwa kuwakandamiza, kuwanyanyasa na kuwaumiza wengine kimwili na kihisia kinyume sheria na taratibu za nchi na pia kiunyume na mafundisho ya dini zote. Vitabu vitakatifu vinaeleza kuwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo ni lazima maisha yetu yaenzi kusudi la uumbaji wa Mungu la kuishi kwa upendo, furaha kuwa sababu ya wengine kufurahia maisha.” Alisema Mameo.
Askofu Mameo aliongeza kuwa watawala kote nchini waombe Mungu ili wasiwe chanzo cha kunyanyasa na kuumiza wengine kwa kuwa wana madaraka. Alisema kuwa jamii ya Kitanzania na kote Duniani iungane na kusema hapana dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwani vitendo hivyo huacha makovu makubwa yasiyofutika kwa wahanga.
Akizungumza kwenye kongamano hilo lililowaleta pamoja viongozi wa dini, wanasheria, maafisa usatwi wa jamii wa Manispaa ya Morogoro na waandishi wa habari, mratibu wa Mipango wa KKKT Dayosisi ya Morogoro, Yona Kitua, alisema kuwa jamii ienedelee kuelimishwa kwa lengo la kubainisha vitendo vipi vinaangukia katika ukatili wa kijinsia, madhara na nini kifanyike kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia visiendelee kutokea.
“Ili jamii iwe salama pasipo vitendo vya ukatili wa kijinisia, lazima tuendelee kutoa elimu kwa mbinu mbali mbali na bila kuchoka, kwani elimu ndio njia pekee inayoweza kubadili tabia na mienendo isiyofaa kwenye jamii.” Alisema Yona.
Afisa Utawi wa Manispaa ya Morogoro, Fidna Mathias, alisema kuwa hakuna sababu ya jamii kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwataka watu wote wanaofanyiwa vitendo hivyo au wanaoshudia mtu anafanyiwa vitendo hivyo kuripoti kwenye mamlaka husika.
Naye Omary Hussen Mwandishi wa habari wa kituo cha Star TV Morogoro, mmoja wa waandishi waliohudhuria kongamano hilo, alisema kuwa dhima kubwa ya vyombo vya habari ni kusambaza elimu kwa jamii, hivyo waaandishi wa habari wanapaswa kuhakikisha ujumbe unaotolewa kuhusu kupinga vitendo vya ukatali wa kijinsia unaifikia jamii yote.
Aliwaasa waandishiwa wa habari kote nchini, kuzitumia siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kuandaa, makala na vipindi mbali mbali vya kuelimisha jamii kuendeleza mampambano ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇