LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 31, 2023

RAIS WA UJERUMANI KUZURU MAKUMBUSHO YA VITA VYA MAJIMAJI MJINI SONGEA, KESHO

Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Dk. Frank-Walter Steinmeier, kesho Novemba Mosi, 2023.
anatarajiwa kutembelea Songea mkoani Ruvuma, kuona Makumbusho ya kumbukumbu ya Vita vya Majimaji vilivyotokea wakati wa ukoloni wa Wajerumani.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas, baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Songea Raisn Dk Frank-Walter Steinmeier, ataenda moja kwa moja katika Makumbusho hiyo ambako atapata historia na kutoa heshima kwa mashujaa waliokufa katika vita hivyo vilivyopiganwa mwaka 1905- 1907.

Kanali Thomas ameongeza kuwa pamoja na kutoa heshima Rais huyo atakutana na baadhi ya walioathirika na vita hivyo na pia atatembelea Shule ya Msingi Majimaji.

Rais Dk. Frank-Walter Steinmeier yupo Tanzania kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia kuanzia leo hadi kesho Novemba Mosi, 2023.

Rais Dk. Frank-Walter Steinmeier

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages