LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 8, 2023

KOMREDI CHONGOLO ATAKA UPUNGUFU WA MAJI NAMANYERE, NKASI UBAKI HISTORIA

Katibu Mkuu wa CCM Komredi Daniel Chongolo akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Shina namba 3, Zakaria Shoma Katibu Mji wa Namanyere, wilayani Nkasi, Rukwa Oktoba 8, 2023 wakati wa siku ya kwanza ya ziara ya kuimarisha uhai wa CCM, kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama.

Akizungumza katika kikao hicho na kusikiliza kero zao, Komredi Chongolo ametoa ahadi ya kwenda kumueleza Rais Samia Suluhu Hassan Ili kuitafutia ufumbuzi changamoto ya maji katika Mji wa Namanyere Ili ibaki kuwa historia.

 Aidha ameiagiza Wakala wa Umeme Vijijini REA kuhakikisha wanakamilisha haraka usambazaji wa Umeme katika vijiji vichache vilivyobakia wilayani Nkasi. 





Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, Bupe Mwakang'ata (kushoto), akiwa katika kikao hicho.

Mwenyekiti wa Shina hilo, Shoma akifungua kikao.



Mbunge wa Nkasi Kusini, Mbogo akielezea kero mbalimbali zinazoikabili Wilaya ya Nkasi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere akizungumza wakati wa kikao hicho.

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
  

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages