LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 4, 2023

CHONGOLO ASHITUKIA KUSUASUA UJENZI WA BARABARA YA KIBAONI-STALIKE MLELE







 

 Na Richard Mwaikenda, Mlele


Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Daniel  Chongolo ameshitukia kusuasua kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Kibaoni-Stalike  hivyo kuagiza uongozi wa wilaya ya Mlele ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga kukutana na uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Kampuni ya ushauri na mkandarasi Ili  kuhakikisha kasi ya ujenzi inaongezeka. 



Chongolo ametoa agizo Hilo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo  iliyopo wilayani Mlele, Katavi Oktoba 4,2023, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.


 Wakati wa kuhitimisha ziara yangu Oktoba 7, 2023, nitamuita Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa aje kukagua Maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na kuwaeleza wananchi ni namna gani barabara hiyo itakamilishwa kwa spidi."


 Barabara hiyo yenye urefu wa zaidi ya Km 50 inayogharimu zaidi sh. Bil. 80, inajengwa na Kampuni ya China ya CRSG. Ujenzi wa barabara ulianza Juni 23, 2022 na inatakiwa ukamilike Juni 22, 2925.


Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Katavi, Albert Laizer  kuhusu Maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo, amesema kuwa umefika asilimia 11.2 nyuma ya utekelezaji  ambao ulipaswa uwe asilimia 21. Muda umefika miezi 15 kati ya 36 iliyopangwa. Hadi sasa mkandarasi ameshalipwa kianzio zaidi ya sh. Bil. 12.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages