Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Daniel Chongolo akimpongeza Mwenyekiti wa Shina namba 5 Tawi la Kapalamsenga, wilayani Tanganyika alipokwenda kuhudhuria kikao cha shina hilo wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kusikiliza kero za wananchi pamoja na kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
Chongolo akitia saini kwenye kitabu cha wageni alipowasili kwenye shina hiloKatibu wa NEC Oganaizesheni wa CCM, Issa Haji Gavu akielezea umuhimu wa kujiunga CCM na kupata kadi za kidijitali za chama hicho.
Mwenyekiti wa shina Michael Lugelelo akififungua kikao cha shina kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo,
Baadhi ya wanachama wa shina hilo wakishabgilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi baadhi ya changamoto zinazowakabili katika shina hilo likiwemo la mgogoro wa wakulima nawafugaji.
Komredi Chongolo akihutubia katika kikao cha shina hilo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇