KIWANGWA, CHALINZE
Mbunge wa Chalinze na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Ndg. Ridhiwani Kikwete amefanya ziara fupi katika kata ya Kiwangwa kuongea na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali ya Kijiji kuhusu shughuli ya maendeleo katika eneo hilo.
Katika kikao hicho pamoja na mengine mengi , Mbunge wa Chalinze Ndg. Kikwete alitumia fursa hiyo kukabidhi mifuko 200 kwa serikali ya kijiji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne katika shule ya Sekondari ya Ridhiwani Kikwete inayojengwa katika Kijiji cha Kiwangwa, Kata ya Kiwangwa. Akizungumza katika kikao hicho, Mbunge aliwashukuru wadau mbalimbali wanaochangia maendeleo katika halmashauri hiyo na kuwahimiza wadau wengine wanaoguswa kuchangia shughuli mbalimbali na si kusubiri serikali. Mbunge alitumia nafasi hiyo pia kuwaomba viongozi kuhakikisha wanasimamia ujenzi na thamani ya michango hiyo ionekane kwa faida ya jamii tunayoiongoza.
Akizungumza baada ya kupokea mifuko hiyo ya Theruji, Diwani wa kata hiyo Ndg. Malota Kwaga amemshukuru Mbunge na kuwaomba viongozi wenzake kuendelea kumuunga mkono Mbunge kwa kazi nzuri anazozifanya akishirikiana na uongozi mzuri wa Rais wetu Dr. Samia Suluhu Hassan. Akizungumza Ndg. Diwani aliwakumbusha juhudi mbalimbali anazofanya Mh. Rais kwa ajili ya watu wa Kiwangwa na Chalinze ni za kipekee huku akishukutu serikali kwa fedha zaidi ya shilingi Bilioni 2 zilizopelekwa katika kata hiyo kwa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo zahanati, shule ya sekondari , umeme, maji n.k.
Baada ya kumaliza ziara ya Shuleni hapo, Ndg. Kikwete alikwenda kutazama zahanati ya Kiwangwa ambayo inapangwa kupanuliwa kuwa kituo cha Afya ili kuhudumia wananchi wa kata hiyo. Akizungumza Mbele ya Mbunge , Diwani Malota alimwambia Ndg. Mbunge kuwa, zahanati hiyo inapokea wagonjwa zaidi ya 3000 kwa wiki hivyo kuwa moja ya zahanati zinazohudumia watu wengi ukizingatia kuwa shughuli za kilimo zinafanyika sana katika eneo hilo.
#KaziInaendelea #Kiwangwa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇