LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 26, 2023

DC MGENI AONGOZA KIKAO KAMATI YA USALAMA KUJADILI MAPATO SAME

 



Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni ameongoza wajumbe wa kamati ya Usalama wa Wilaya hiyo kwenye kikao cha kwanza kujadili mapato kutoka taasisi mbalimbali za serikali, ambapo Pamoja na mambo mengine ameagiza kikao hicho kufanyika Kila mwezi.


Amesema malengo ya kutaka kikao hicho kufanyika Kila mwezi ni kuongeza ufuatiliaji kuhakikisha taasisi zote zinafikia malengo kwenye kukusanya mapato pia kutafuta ufunguzi wa haraka inapobainika Changamoto inayoweza kukwamisha zoezi hilo ambapo wajumbe wa kamati ya usalama watapokea taarifa za makusanyo Kwa Kila taasisi Kujua mwenendo wa makusanyo kila mwezi. 


Taasisi ambazo ni wajumbe wa kikao hicho ni Pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Same, Mamlaka ya mapato nchini (TRA), hifadhi ya Taifa Mkomazi, Mamlaka ya usimamizi wa wanyama Pori  nchini (TAWA). Wakala wa kudumu za Misitu Tanzania (TFS) na Wakala wa Maji safi na usafi wa mazingira vijijini  RUWASA.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages