Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, amesema hatua thabiti iliyochukuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuboresha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kuiwezesha fedha za kutosha ndiko kumeleta neema kwa wastaafu sasa kulipwa mafao yao kwa wakati tofauti na zamani.
Alisema kabla ya Rais Dk. Samia kuchukua hatua ya kuiwezesha kifedha Mifuko ya Hifaghi ya Jamii kupitia Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza, wastaafu wengine walikuwa wanakaa hadi miaka miwili hawajapata pesheni kutokana na hali mbaya ya kifedha katika mifuko hiyo ambayo ilitokana na madeni ya serikali ambayo yalikuwa hayajalipwa.
Prof. Ndalichako alisema, baada ya Rais Dk. Samia ukwasi uliokwamisha wastaafu kulipwa kwa wakati kutokana na serikali kuwa na deni la sh. trilioni 4. 6 zilziotokana na watumishi walioingizwa kwenye mfumo wa pensheni lakini wakawa hawachangii, serikali ikaahidi ingewachangia, lakini tangu 1999 hadi 2021 ilikuwa haijalipwa ndipo Rais Dk. Samia akaamua kutoa sh. trilioni 2.17 kama hati fungani na kulipa sh. bilioni 500 kati ya Sh. bilioni 731 za madeni yaliyotokana na uwekezaji katika maeneo mbalimbali ya serikali ambayo aliyakuta.
Aliyasema hayo wakati akifungua semina ya siku mbili ya kuwajengea uelewa katika nyanja mbalimbali Wastaafu watarajiwa 281 kutoka Taasisi mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam, wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) iliyoanza Septemba 11, 2023.
Prof. Ndalichako alisema, kufuatia hali bora ya kifedha katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ndiyo maana sasa yeye na watendaji wa Mifuko hiyo wanazungumza kwa kujiamini kuwa wastaafu wanaweza kulipwa pensheni zao kwa wakati ili kukidhi dhamira ya Rais Samia.
Aliipongeza PSSSF kwa kuandaa semina hiyo iliyobeba kauli mbiu 'Wekeza Mafao yako Sehemu Salama kwa Uhakika wa Ukwasi', kusudi likiwa kuwajengea wastaafu wake watarajiwa uelewa na ufahamu juu ya umuhimu wa kufanya maamuzi sahihi ya kukuza vipato vyao baada ya kustaafu ili kuleta tija na uendelevu wa kipato.
“Wosia wangu kwenu ni kuyatumia vyema madini ya elimu mtakayoyapata hapa kwa kushikilia mambo makuu matatu ambayo ni kuwa na mtazamo chanya, kuweka mipango makini na kutimiza ndoto binafsi baada ya kustaafu na kustaafu ni wajibu kwa kila mtumishi hivyo hakuna budi kuendeleza maisha mazuri hata baada ya kustaafu", alisema Prof. Ndalichako.
Alisema ni vema mtumishi akatambua kuwa safari ya kustaafu inaanza pale anapoanza ajira, hivyo ni muhimu kujiandaa kimipango na kifedha ili kufurahia maisha ya uhuru lakini lazima kuwa na umakini katika usimamizi wa fedha.
Mapema, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema PSSSF inatarajia kuwa na wastaafu 11,000 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 na hadi sasa inao wanachama 739,000, na kuongeza kuwa katika Suala la mazingira PSSSF inalenga kila mmoja kupanda na kuutunza mche atakaopewa na Mfuko huo wakati wa akustaafu.
CPA Kashimba alisema, Semina kama hiyo zilianza kufanywa na PSSSF ambapo ya kwanza ilifanyika mwaka 2021 kwa wastaafu watarijiwa 3700 bara na Zanzibar, na mwaka huu pia elimu itawafikia wastaafu kwenye mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Alisema katika Semina Wastaafu watarajiwa wanapatiwa mafunzo ya elimu ya uwekezaji katika masoko ya fedha, taarifa za nyaraka na utaratibu wa kufuata wakati wa kustaafu, kujiandaa kisakolojia baada ya kutoka kwenye utumishi, umuhimu wa kutunza mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, na uhalifu wa kimtandao ambao unawaathiri wastaafu wengi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, akifungua semina ya siku mbili ya kuwajengea uelewa katika nyanja mbalimbali Wastaafu watarajiwa kutoka Taasisi mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam, wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) iliyoanza Septemba 11, 2023. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, akiwasili kufungua semina ya siku mbili ya kuwajengea uelewa katika nyanja mbalimbali Wastaafu watarajiwa kutoka Taasisi mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam, wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) iliyoanza Septemba 11, 2023. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, akiingia ukumbini kufungua semina ya siku mbili ya kuwajengea uelewa katika nyanja mbalimbali Wastaafu watarajiwa kutoka Taasisi mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam, wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) iliyoanza Septemba 11, 2023. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, na kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Mbaruku Magawa,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako, akiwa meza Kuu baada ya kuingia ukumbini kufungua semina ya siku mbili ya kuwajengea uelewa katika nyanja mbalimbali Wastaafu watarajiwa kutoka Taasisi mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam, wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) iliyoanza Septemba 11, 2023. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba,Baadhi ya Viongozi wa Menejimenti ya PSSSF wakimlaki Prof. Ndalichako ukumbini.
Washiriki wa Semina wakimlakini Prof. Ndalichako ukumbini.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, James Mlowe, akiongoza semina hiyo akimkaribisha Prof Ndalichako ukumbini..Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Mbaruku Magawa, akizungumza mwanzoni mwa semina hiyo. Kulia ni Prof. Ndalichako na CPA Kashimba.Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, akizungumza kwenye semina hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, akipongezwa na Prof. Ndalichako baada ya hotuba yake.Prof. Ndalichako akizungumza kwenye Semina hiyo.
Mstaafu Mtarajiwa Juliana Haule ambaye ni Mhasibu Chuo Kikuu cha Ardhi akitoa neno la shukurani baada ya hotuba ya Prof. Ndalichako.
Wastaafu watarajiwa wakigawiwa miche ya miti ya matunda na Prof Ndalichako.👇
========================
Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo👇
==================
Picha za Kumbukumbu👇

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇