LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 6, 2023

MAMA MARIAM MWINYI AITAKA JAMII KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MWANI NA FURSA ZAKE KIUCHUMI.

Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu  na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi ameitaka jamii kujikita zaidi kwenye kilimo cha zao la Mwani kwani kina fursa nyingi za uchumi na maendeleo.

Mama Mariam Mwinyi ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Kimataifa unaojadili mifumo ya chakula  barani Afrika  katika mada ya nafasi ya Mwanamke kwa sekta ya kilimo na chakula, iliyofanyika ukumbi wa Selous jengo  la ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere.

Vilevile, amesema Taasisi ya ZMBF imewawezesha kiuchumi Wanawake wakulima wa Mwani baada ya kuwaweka pamoja vikundi 16 vya kina mama kila kikundi  20 kwa Unguja na Pemba kwa kuwapa mikopo nafuu ili kuendeleza zao hilo.



No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages