*
Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa kufunga Kikao Kazi cha Taasisi Simamizi za Madili katika Utendaji, Kitaaluma na Watumishi wa Umma kutoka Wizara na Taasisi za Umma kilichofanyika katika ukumbi wa PSSSF Jijini Dodoma.
"Nimatarajio yangu kuwa ninyi kama wawakilishi wa watumishi katika Taasisi zenu, mtakuwa chachu kwa wengine katika uzingatiaji wa maadili" alisema.
Mhe. Kikwete aliongeza kuwa maadili mema ni msingi mkubwa katika utoaji haki, hivyo Watumishi wa Umma wazingatie maadili ili haki itendeke wakati wote wa utoji huduma.
Vilevile, aliwakumbusha washiriki kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi katika sehemu zao za kazi na zaidi kuwa kiungo kizuri kati ya Serikali na Wananchi katika utoaji huduma bora.
Mhe. Kikwete amewasisitiza Watumishi wa Umma kuhakikisha wanatatua malalamiko ya Wananchi ili kuwapunguzia viongozi wa kitaifa kutatua malalamiko ambayo yangeweza kutatuliwa katika sehemu zao za kazi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇