Na Richard Mwaikenda, Dodoma
BARAZA Kuu la Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), limeazimia kuihamisha akaunti kuu ya Chama hicho kutoka Benki yao ya Mwalimu Commercial Bank (MCB) kwenda Benki ya NMB.
Uamuzi huo umefanywa na wajumbe wa baraza Hilo baada ya kupiga kura katika mkutano maalumu uliofanyika makao Makuu ya chama hicho, jijini Dodoma Septemba 25, 2023.
Mkutano wa Baraza hilo linaloundwa na wenyeviti wa CWT wa Wilaya na mikoa uliongozwa na Rais wa CWT, Leah Ulaya ambaye baada ya kura kupigwa alitangaza kuwa maazimio hayo yatafanyiwa kazi.
Uamuzi huo wa kuhamisha akaunti umekuja kufuatia tafrani iliyotokea hivi karibuni baada akaunti yao Kuu kusimamishwa kwa muda wa takribani wiki mbili kupisha mgogoro wao na aliyekuwa kaimu mhasibu mkuu ambaye kupitia Wakili wake kudai kuwa ana haki ya kuendelea na kazi yake hiyo.
Rais wa Chama cha Walimu Nchini (CWT), Komredi Leah Ulaya, akifungua kikao cha Baraza Kuu la chama hicho cha Dharula kilichofanyikia Makao Makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Japheth Maganga na Kulia ni Makamu Rais wa Chama hicho, Suleimani Ikombe. Kikao hicho pamoja na mambo mengine wameridhia maadhimisho ya miaka 30 ya chama hicho tangu kianzishwe Novemba 1.1993 kitafanyika mkoani Mwanza ambapo walimu zaidi ya 60,000 wanatarajiwa kuhudhuria. Pia wameazimia kuhamisha akaunti yao kuu tkutoka benki yao ya MCB kwenda NMB.Katibu Mkuu wa Chama hicho Komredi Japheth Maganga, akitoa maelezo kwa wajumb e wa kikao
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa kikaoni
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇