LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 23, 2023

SERIKALI YAONYA WANAOTAPELI KUWAREJESHA KAZINI WALIOFUKUZWA KWA KUGHUSHI VYETI

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Serikali imetoa onyo kwa matateli ambao wamekuwa akitumia mitandao ya kijamii kupotosha kuwa wanao uwezo wa kuwajesha kazini Watumishi wa Umma waliofukuzwa kazi kwa kosa la kughushi vyeti na waliosimamishwa kazi kwa kutokuwa na vyeti ya kidato cha nne mwaka 2012-2019.

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utwala Bora, mbali na kutoa onyo kwa matapeli hao, pia imetahadharisha Watumishi wa Umma na wananchi kwa jumla kuwa makini na taarifa hizo kwa kuwa Serikalai ina njia na utaratibu rasmi wa kutoa taarifa kwa wadau wake na sio utaratibu huo unaotumiwa na matapeli hao.

"Kumekuwa  na mfululizo wa uandaaji wa taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii kuhusu urejeshwaji wa watumisi walioondolewa kwenye utumishi wa umma kwa kosa la kughushi vyeti na waliosimamishwa kazi kwa kutokuwa na acheti cha kidato cha nne mwaka 2012-2019.

Wapotoshaji hao wanawataka watumishi waliosimamishwa/kufukuzwa kazi Serikalini kuwasilisha nyaraka mbalimbai ikiwa pamoja na nakala ya barua ya kushinda rufaa, kitambulisho cha NIDA, barua ya kuthibitishwa kazini, salary slip na barua ya kusimamishwa/kufukuzwa kazi na wanaombwa kutoa kiwango fulani cha fedha kadri ya makubaliano ili warudishwe kazini," imesema taarifa iliyotumwa kwetu na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Utumishi) Mary Mwakapenda.

Taarifa hiyo imesema, matapeli hao wamekuwa wakinbadili tarehe ya taarifa yao kwa umma na kuacha maudhui yakiwa ya aina moja na kuwataka Watumishi husika kuwasiliana nao kwa namba za simu +255 627 416394, +255 621 86 163 au +255 735 051 419 kwa alengo la kujipatia kipato kwa njia ya udanganyifu.

Hivyo, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utwala Bora inawasisitizia Watumishi wa Umma na wananchi kwa jumla kuwa makini na taarifa hizo kwa kuwa Serikalai ina njia na utaratibu rasmi wa kutoa taarifa kwa wadau wake na sio utaratibu huo unaotumiwa na wapotoshaji hao.

Aidha, Serikali inatoa onyo kwa wapotoshaji hao kucha tabia hiyo kwa kuwa kupitia vyombo vyake vya dola inaendelea kufatilia ili kuwabaini na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa sheria.


 TAARIFA YA SERIKALI👇

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages