Na Bashir Nkoromo, CCM Blog.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, amewapangia vituo vya kazi Mabalozi aliowateua Mei 10, 2024 na kuwabadilisha vituo vya kazi Mabalozi wanne.
Taarifa ya Ikulu imewataja Mabalozi waliopangiwa vituo vya kazi ni Balozi Fatma Mohd Rajab aliyepangiwa Oman badala ya Balozi Aabas Kilima anayestaafu na Balozi Joseph Edward Sokoine nchini Canada badala ya Dk. Mpoki Ulisubisya anayestaafu, huku Balozi Naim Sweetie Hamza Aziz akipangiwa nchini Australia.
Taarifa imesema, Rais amemteua kuwa Balozi Meja Jenerali Ramson Godwin Mwasika na kumpangia kwenda nchini Rwanda, badala ya Meja Jenenerali Richard Mutayoba Makanzo aliyehamishiwa Cairo, Misri na kumteua kuwa Balozi Gelastus Gasper Byakanwa kisha kumpangia kwenda Burundi badala ya Jilly Maleko liyestaafu.
Rais amemteua pia kuwa Balozi Habibu Awesi Mohamed na kumpangia kwenda Qatar badala ya Balozi Mahadh Juma Maalim aliyemhamishia Kuala Lumpur, Malaysia na kumteua Imani Salum Mjalikali kisha kumpangia kwenda Algeria badala ya Meja Jenerali Jacob Gideon Kingu aliyestaafu.
Pia Rais amemteua kuwa Balozi Hassan Iddi Mwamweta na kumpangia kwenda Ujerumani badala ya Abdallah Salehe Possi aliyemhamishia Geneva Uswisi pia Rais akimteua kuwa Balozi Dk Mohamed Juma Abdallah na kumpangia Saud Arabia badala ya Balozi Ali Jabir Mwadini anayeenda Paris, Ufaransa.
Taaraifa imewataja waliohamishwa vituo kuwa ni, Balozi Ali Jabir Mwadini aliyehamishiwa Ufaransa, badala ya Balozi Dk. William Shelukindo aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Usgirikiano wa Afrika Mashariki.
Aidha Balozi Meja Jenerali Richard Mutayoba Makanzo Rais amemhamishia kwenda Misri badala ya Balozi Dk. John Emmanuel Nchimbi anayerejea nyumbani, huku Balozi Abdallah Possi akimhamisha kwenda kuwa Mwakilishi wa Kudumu Ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) Geneva Uswisi badala ya Maimuna Tarishi aliyemaliza mkataba.
Taarifa imekamilisha ikisema Balozi Dk. John Stephen Simbachawene amehamishiwa nchini Uganda badala ya Balozi Azizi Mlima anayestaafu na kwamba Mabalozi wateule wataapishwa Agosti 15, 2024 saa 5 asubuhi. Ikulu, Chamwino, Dodoma.
Your Ad Spot
Aug 11, 2023
Home
featured
Kitaifa
RAIS DK. SAMIA AWAPANGIA VITUO MABALOZI ALIOWATEUA, WANNE AWABADILISHA VITUO, DK. NCHIMBI KUREJEA NYUMBANI
RAIS DK. SAMIA AWAPANGIA VITUO MABALOZI ALIOWATEUA, WANNE AWABADILISHA VITUO, DK. NCHIMBI KUREJEA NYUMBANI
Tags
featured#
Kitaifa#
Share This
About CCM Blog
Kitaifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇