LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 6, 2023

OLE WENU MNAOTENGENEZA MIGOGORO YA ARDHI MPATE RUSHWA-DC SAME

 



 Mkuu wa wilaya ya same kasilda mgeni amewaonya viongozi wa serikali za vijiji dhidi ya tabia iliojikita kwa baada yao ya kutengeneza migogoro hasa ya ardhi ikiwa ni sehemu ya kujipatia kipato.


Kasilda amesema amebaini maeneo mengi yenye migogoro imetengenezwa na baadhi ya viongozi hao kwa maslahi binafsi hali ambayo inapelekea wananchi kutoiamini serikali yao 

Ameyasema hayo  katika mwendelezo wa ziara zake za kusikiliza kero za wananchi  ambapo wakati huu ameifikia kata ya makanya .


Akihutubia wananchi amesema viongozi hao wajue kuwa wana dhamana  ya kuhakikisha wanamsaidia mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samiha Suluhu Hassani kutatua kero zinazowakabili wananchi na si kuwa chanzo cha kero  na migogoro kwa wananchi .


Dc Kaslida aliendelea kusema migogoro ya ardhi ambayo wananchi wanailalamikia kwenye kata hiyo kwa kiwango kikubwa  imesababishwa na  baadhi viongozi  wasio waadilifu   Kwa kuuza Ardhi kiholela kinyemela huku wananchi wakiendelea kudanganywa kuwa maeneo hayo yamevamiwa na wageni .



Amesema serikali haiwezi kuvumilia kuwa na viongozi wa  namna hiyo ,kama hawawezi kubadilika wakae pembeni kabla hawajaondolewa

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages