LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 6, 2023

MWENYEKITI CCM KYERWA AKERWA NA UPOTOSHAJI

 


 Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kyerwa Daniel Damian akizungumzia katika kikao cha Baraza Kyerwa

Na Lydia Lugakila,

KYERWA


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera Daniel Damian amewataka viongozi wa Chama hicho Wilayani Kyerwa kutokubaliana na baadhi ya watu wanaopita pita na kupotosha Umma wa Watanzania kwa mambo wasiyokuwa na uelewa nayo.


Daniel Alitoa kauli hiyo katika kikao cha Baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa alipopewa nafasi ya kutoa salamu za Chama.


"Kwa wakati kama huu sisi kama Chama tunaangalia mbele tunaenda kwa matendo maneno hayafai" alisema kwani kuna baadhi ya watu wanajitoa muhanga kupotosha kwa baadhi ya mambo Mwenyekiti wa CCM Kyerwa.


Aliwaomba viongozi wa chama hicho na Wanachama kuwaepuka kukaa mbali na wapotoshaji wanaotoa kauli mbali mbali wasizokuwa na uhakika nazo ikiwemo suala la bandari.


"Namshukuru Rais Samia juu ya suala la bandari lengo lake ni kubwa kwa Watanzania kwani anahitaji bandari iingize mapato ya kutosha na kuwasogeza karibu wawekezaji lakini wasioyaelewa malengo wanakuja kwa maneno wakiamini kuwa lengo ni bandari kuuzwa wakati ni kuboreshwa  jiepusheni nao" alisema Daniel.


Aidha aliwapongeza viongozi wa Halmashauri hiyo wa Chama na Serikali kutokana na kazi kubwa iliyofanyika ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho na kuwa chama kimelidhika kwa kiwango kikubwa.


Hata hivyo aliwahakikishia madiwani hao kuwa nao bega kwa bega huku akiwapongeza kwa kazi pamoja na mbunge wa Jimbo hilo Innocent Seba Bilakwate ambaye anafanya vizuri ambapo ameeleza kuiona kazi iliyofanyika  katika ukusanyaji wa mapato kwa Halmashauri hiyo na kuwaomba viongozi wa dini kuzidi kuliombea taifa ili amani iendelee kuwepo.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages