Katika kikao cha Baraza la Uwt mkoa wa Dar es salaam kilichoketi leo tarehe 04/8/2023 Ukumbi wa Idd Nyundo katika manispaa ya Temeke Mwenyekiti Uwt Mkoa Cde Mwajabu Mbwambo.
Amewahimiza wajumbe wabaraza hilo ambao wamebahatika kupata mafunzo ya semina mbalimbali ili kuwajengea uwezo kuhakikisha wanabadilika na kutekeleza kwa matendo ili waweze kuwa bora zaidi na kuhakikisha wanasimamia mambo yanayohusiana na wanawake na watoto ndani ya mkoa wa Dar es salaam. Ambayo Rais Dr Samia Suluhu Hassan ameweka miundo mbinu mbalimbali ya kuwakwamua mwanamke katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na mpango wa kutokomeza na Ukatili wa kijinsia, miundo mbinu ya afya, lishe, elimu, maji na utunzaji wa mazingira kwa kupitia matumizi ya nishati safi.
Mwenyekiti Cde Mwajabu, amewakumbusha kuhakikisha wanatekeleza mpango kazi wa Uwt ambao unatoa maelekezo jinsi ya kuhuisha uhai wa jumuiya na chama, kutatua changamoto za wanawake na watoto mfano kwenye masuala ya kisheria. Kutoa mafunzo ya uwezeshaji wa wanawake ili kujikwamua kiuchumi na utafutaji wa fursa na kuwajengea wanawake uwezo na kuwahamasisha lugombea nafasi mbalimbali za uongozi ifikapo 2024.
Mwenyekiti wa Uwt Mkoa Dar es salam Mwajabu Mbwambo amewaasa wajumbe wa baraza kuwa ili kuleta mabadiliko ndani ya mkoa wa Dar es salaam ngazi zote za uongozi ni lazima kuujua mpango kazi na kuutekeleza kwa vitendo na kuuishi ili kuunga juhudi zinazofanywa na serikali ya Rais Dr Samia kwenye masuala ya wanawake na watoto.
Mwenyekiti aliwaagiza wenyeviti na makatibu wa wilaya, wabunge viti maalum na madiwani viti maalum kuhakikisha wanaelimisha Wanawake katika suala la uwekezaji wa bandari ya Dar es salaam kuepusha upotosbaji ili kumuunga mkono Rais Dr Samia Suluhu Hassan katika kuleta maendeleo ya taifa letu kiuchumi.
Katika Kikao hicho cha baraza wabunge wa Viti maalumu mkoa wa Dar es salaam waliwasilisha utekekelezaji wa ilani kwa
kipindi cha miezi sita. Na wamejikita katika mausuala yanayowahusu wanawake na watoto.



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇