LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 29, 2023

KAWE UKWAMANI SEC. WAFUNDWA KUFUATA NYAYO ZA RAIS DK. SAMIA NA MAKAMU DK. MPANGO

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Wanafunzi Shule ya Sekondari Kawe Ukwamani Jijini Dar es Salaam, wamehimizwa kuzingatia masomo kwa bidii na kuachana na yasiyowahusu kwa sasa ili badaye miongoni mwao wawe viongozi makini kama Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango.

Sanjari na Wanafunzi, Wazazi na walezi nao walihimizwa kuwaangalia watoto kwa karibu ili kuhakikisha hatumbukii katika anasa na vitendo vibaya ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya, umalaya kwa kuwa watoto wasipochungwa vema wanaweza kukumbwa na vitendo hivyo na kukwamisha ndoto zao.

Hayo yalisemwa kwa nyakati tofauti na Diwani wa Kata ya Kawe, Muta Lwakatare na Mkuu wa shule hiyo Safina Egha katika mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika juzi katika shule hiyo, ambapo jumla ya Wanafunzi 378 wanatarajiwa kuhitimu baada ya kufanya mitihani yao Novemba mwaka huu.

"Hatua mliyofikia ni ya kujivunia, lakini msidhani ndiyo mwisho, kwanza hakikisheni siku ya kufanya mitihani kila mmoja wenu amtangulize Mungu mbele na kisha mhakikishe mnakuwa makini, msiwe na papara katika kujibu maswali na baada ya mitihani endeleeni kuyashika masomo na maadili mliyopewa na walimu wenu hawa", alisema Diwani Lwakatare na kuongeza;

"Ninyi wakike, bila shaka mnaona Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan alivyo mchapakazi tena makini, hii yote ni kwa sababu alizingatia kusoma kwa bidii na kuachana na yasiyomsuhu kwa wakati ule, sasa na ninyi fuateni nyazo zake baadhi yenu au wote mje kuwa viongozi bora katika taifa letu, na ninyi wa kiume fuateni nyayo za Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango mje kuwa kama yeye".

Akizungumza kabla ya Diwani Lwakatare,  Mkuu wa Shule hiyo Safina Egha aliwazindua Wazazi akiwambia katika kulianda watoto ulindaji uwe sawa kwa wakike na wakiume, baadala ya baadhi yao kukazana kulinda wa kike wakidhani wakiume wapo salama, akisema wakiume nao siku hizi ndiyo wapo katika majanga ikiwemo kuingizwa katika mitandao miovu na kulawitiwa.

"Na ninyi wanangu nawasihi sana, acheni kutamani kuvuka daraja kabla hamjalifikia, mkitaka mje kuwa na maisha mazuri na viongozi bora baadaye, zingatieni masomo tu, mambo mengine yote hata kama ni mazuri mtakuja kuyakuta baadaye", alisema Mkuu Egha.

 

Kuhusu ufanisi wa shule,  Mkuu Egha alisema mwaka jana zaidi ya nusu ya wahitimu wa kidato cha nne walifanya vema katika shule hiyo na kuendendelea na masomo.

 

Na kuhusu watoto wenye ulemavu, Mkuu Egha aliwaomba wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka shule watoto hao badala ya kuwaficha.

Diwani Kata ya Kawe, Muta Lwakatare, akimkabidhi cheti mhitimu mtarajiwa Maya Bashir Nkoromo,  katika Mahafali ya Kidato cha Nne yaliyofanyika juzi, Shule ya Sekondari Kawe Ukwamani, Dar es Salaam, Jumla ya Wanafunzi 378 walipata vyeti na kuvirejesha ili kupea rasmi baada ya kumaliza mitihani ya kuhitimu kidato hicho Novemba mwaka huu. Wapili kulia ni Mkuu wa shule hiyo Safina Egha akifuatiwa na Makamu Mkuu Peter Chacha.

Picha kuanzia mwanzo wa sherehe ya Mahafali hayo👇

Mwalimu Peter John akiandaa kupata chakula kwanza wahitimu watarajiwa wa Kidato cha nne, kabla ya kuanza rasmi sherehe ya Mahafali yao, yaliyofanyika Oktoba 24, 2023, katika shule ya sekondari Kawe Ukwamani, Jijini Dar es Salaam.
wahitimu hao watarajiwa wakipata chakula.
Mgen rasmi katika Mahafali hayo, Diwani kata ya Kawe Muta Lwakatale akiwasili shuleni.
Mkuu wa Sekondari ya Kawe Ukwamani Safina Egha akiwa ofisini kwake na mgeni rasmi, wakati mgeni huyo akisaini kitabu cha wageni pamoja na ujumbe wake,
Katibu Mtendaji Kata ya Kawe Husna Nondo akimsaidia Diwani Muta kusaini Kitabu cha wageni.
Wazazi, Walezi na waalikwa wakisubiri sherehe hiyo kuanza.
Mgeni rasmi Diwani Muta Lwakatare akiongozana na Mkuu wa Shule hiyo Safina Egha kuwasili eneo la tukio.
Wahitmu watarajiwa wakiingia kwa mikogo eneo la mahafali
Wahitimu watarajiwa wakiingia.
Wahitimu watarajiwa wakiingia.
Wahitimu watarajiwa wakiwa wameketi.
Walimu wakiingia kwa mikogo eneo la mahafali.
Kisha walimu hao wakaserebuka muziki baada ya kuingia.
Walimu wote wakajimwayamwaya uwanjani. Katikati ni Mkuu Egha,
Walimu wakiendelea 'kiachia' kila mmoja kivyake.
Diwani Muta naye akawaunga mkono walimu hao kusakata muziki.
Mkuu Egha akamkaribisha Afisa Mtendaji Kata ya Kawe kusalimia.
Afisa Mtendaji Kata ya Kawe akisalimia.
Mwenyekiti wa kamati ya Wazazi ambaye pia ni Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Kata ya Kawe Potipoti Yusufu akisalimia na kufanya utambulisho.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kawe Hemedi Zuberi Gongo akisalimia.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ukwamani Hamisi Chilemba akisalimia.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Muzimuni Raia Nasoro akisalimia
Katibu wa Kamati ya Wazazi Kawe Ukwamani akisalmia.
Mjumbe wa Kamati ya shule akisalimia.Kisha ikafika samu ya Walimu kutoka shule mbalimbali kusalimia.👇
Mwalimu Kajuna kutoka Salma Kikwete Sekondari.
Mwalimu kutoka Bunju Sekondari
Mwalimu kutoka Hananasif
Mwalimu kutoka Michael Tarimo Sec.
Kutoka Makongo Sec.
Magreth Ndosi kutoka Baniel Chongolo Sec
Edith Zongo kutoka Mbezi Sec
Mwalilu kutoka Maendeleo Sec.
Mwalimu kutoka Mikocheni Sec
Mwalimu kutoka Shule ya Msingi Kawe B
Mkuu Egha akitangaza upokeaji wa tuzo kwa walimu mahiri katika ufundishaji masomo. Wakapewa tuzo hizo mmoja baada ya mwingine.👇
👇
👇
👇
👇
👇
👇
👇
👇
👇
----------- Scout nao wakaonyesha uhodari wao👇
Mbinu ya kuona adui akiwa mbali.
Kuanguka kikakamavu.--------
Mwanafunzi mwenye mahitaji maalum akisoma risala.
Diwani Muta akimpongeza mwanafunzi huyo.
Muta na meza kuu wakimzawadia na kumfurahia mwanafunzi huyo.
Wanafunzi wakfanya igizo la Ukombozi.
Mkuu Egha akizungumza kabla ya mgeni rasmi.
Mgeni rasmi akizungumza.
Kabla ya kuendelea kuzungumza mgeni rasmi akaomba uimbwe kwanza wimbo wa utaifa. ukaibwa.
Halafu mgeni rasmi akaomba wote kuserebuka kwanza kufurahia mahafali.
Kisha mgeni rasmi akaendelea na hotuba yake.
Mkuu Egha akizungumza jambo na mgeni rasmi mwishoni mwa sherehe hiyo.
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages