LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 5, 2023

KAMISAA WA CCM DC MPONGOLO NA VIONGOZI WA CHAMA JIMBO LA SEGEREA WAZIDI KUUFUTA UONGO KUHUSU UWEKEZAJI BANDARI

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Buguruni
Kamisaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam Edward Mpogolo, jana aliongoza viongozi wa Chama jimbo la Segerea, kufutilia mbali uongo unaozushwa na wapinzani kuhusu uwekezaji Bandari ambapo badala ya kukiri kwamba ni uwekezaji wanadai bandari hiyo imeuzwa.

Kamisa DC Mpogolo aliongoza Viongozi hao wa CCM, kufututlia mbali uongo huo katika mkutano mkubwa na wa aina yake, uliofanyika Buguruni Sheli, ambao ulihudhuriwa na Mbunge wa jimbo hilo Bonna Kamoli, Katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Dar es Salaam, Ali Bananga, Mwneyekiti wa CCM Ilala  Alhaj Said Side, vingozi mbalimbali wa CCM pamoja na Madiwani wa kata tano za Ilala.

Sanjari na kufuta uongo huo, pia waliweka wazi kwa wananchi ukweli na faida kuhusu uwekezaji huo unaokusudia kutafuta ufumbuzi wa kuimarisha huduma za bandari ya Dar es alaam, ambapo, Oktoba 25, 2022, serikali ilisaini makubaliano na serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kupitia Kampuni ya DP World.

Kwa nyakati tofauti Kamisaa wa CCM DC Mpogoolo na viongozi hao walibainisha kwamba mikataba kati ya Mamlaka ya Bandari (TPA) na DP World bado haijafikiwa na kwamba watalamu wa pande zote mbili wako katika mchakato wa kuitengeneza kwa maslahi ya pande zote.

Walisema katika upotoshaji uliozuka, baadhi ya watu hasa wanasiasa wa vyama vya upinzani wamelivalia njuga suala hilo kwa kuudanganya umma wa Tanzania kwamba bandari ya Dar es Salaam inauzwa wakati siyo kweli kabisa.

Viongozi hao wakiongozwa na Kamisaa DC Mpogolo walisema, serikali ya Tanzania iliingia makubaliano na serikali ya UAE, kuendeleza bandari sio kuuza bandari bali makubaliano yanahusu kuendeleza kiwango cha ufanisi katika bandari ya Dar  es Salaam.

Walibainisha katika mkutano huo kwamba, kwa sasa hali ya ufanisi wa bandari za Tanzania iko chini na bandari ya Dar es Salaam utendaji wake ni wa kiwango kisichotosha ambapo mzigo unapakuliwa kwa siku tano kutoka kwenye meli, wakati viwango vya kimataifa unatakiwa upakuliwe kwa siku moja.

Viongozi hao wa CCM na Kamisaa DC Mpogolo walisema changamoto kubwa katika bandari za Tanzania ikiwemo ya Dar es Salaam ni kukosekana mifumo  ya kisasa ya TEHAMA hali ambayo pamoja na mambo mengine husababisha meli kukaa muda mrefu huku gharama ya meli kusubiri nangani nje ya bandari ikiwa ni sh. milioni 58 kwa siku.

"Kwa hiyo lengo la serikali ni kupunguza muda wa meli kusubiri, kupunguza muda wa kushusha makasha na kupunguza gharama za usafirishaji mizigo kwenda nje,” alisema Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omari Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti'

Walisema Wana CCM wana uhakika DP World italeta mapinduzi ya kiuchumi katika Bandari ya Dar es Salaam na  mbali na kumiliki meli 400 inao uzoefu mkubwa wa kuendesha bandari maana ndiyo inayoendesha baadhi ya banadari kama za Mombasa (Kenya), Walvis Bay (Namibia), Lobito (Angola), Tema (Ghana), na Morocco na inashughilikia asilimia 10 ya biashara ya mizigo duniani.

Viongozi hao na Kamaisaa DC Mpogolo walifafanua kuwa kazi ya kutafuta njia ya kuleta ufanisi katika bandari haijaanza jana wala juzi, ilianza miaka  kadhaa iliyopita kama ilivyokuwa mwaka 2018 ambapo upembuzi yakinifu ulifanywa ili serikali iweze kupata mapato mazuri.

Kwa nyakati tofauti walifafanua kwamba ukomo wa utendaji wa DP World utawekwa katika mikataba ya biashara itakayosainiwa kati  yake na TPA na DP World itasajiliwa hapa nchini  na hisa asilimia 35 zitamilikiwa na wazawa na yenyewe (DP World) itapewa kuendesha asilimia nane tu ya shughuli zote za Mamlaka ya Bandari Tanzania.

"Wana CCM wenzangu ngoja niwaambie, suala hili la uboreshaji wa utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam unaofanyika ni utekelezaji Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025,  Ibara ya 59, ukurasa wa 92,  hivyo kuweni makini na wanaopita kupotosha, kwa sababu wanahofia iwapo CCM ikitekeleza kwa ufanisi kila ilichoahidi kwa wananchi kupitia ilani hiyo yenye kurasa 303, watakosa agenda.

Wapinzani wanapotosha, ili tudanganyike na kuacha uwekezaji huu ili tukose jibu watakapotuuliza wakati wa Uchaguzi kwamba tulifanya nini kutekeleza ilani katika uboreshaji wa Bandari, amkeni Wana CCM msidanganyike hao katika hili wana ajenga ya siri, msidanganyike kamwe,"  alisema  Kamisaa DC Mpogolo.

Akiungana na viongozi wengine katika mkutano huo kulaani wanaomtusi Rais Samia Suluhu Hasaan, kufuatia uwekezaji huo wa Bandari, Kamisaa DC Mpogolo, alisema Rais wahajibu kwa sababu ana akili timamu, busara, hekima na ni mcha Mungu.

"Sisi huko Vijijini wakati Mama yetu kipenzi Rais Samia hajaleta maji, tulikuwa tukienda kuoga mtoni. Sasa unapooga mtoni unavua nguo zako unaziweka kando, akija kichaa akazichukua, wewe unachofanya unachutama, akipita mtu unamuomba nguo unavaa, hutoki uchi kumkimbiza kichaa akupe nguo zako, maana ukifanya hivyo mtaonekana wote ni vichaa wakati wewe una akili zako", akasema Kamisaa DC Mpogolo.

Kimsingi Mkutano huo, ulikuwa umeandaliwa na Mbunge Bona na kwa sababu hiyo, kabla ya viongozi kuamua kufuta uongo wa wapinzani kuhusu uwekezaji bandari, waliutumia mkutano huo kueleza mengi ya maendeleo yaliyofanyika katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia katika jimbo la Segerea.

Kwa nyakati tofauti viongozi hao akiwemo Mbunge Bona walieleza ulivyofanyika ujenzi na uboreshwaji wa miundombinu ya barabara, huduma za elimu, afya na kuboresha hali za wananchi kupitia mikopo kwa kina mama, Vijana na wenye ulemavu,
Kamisaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akizungumza katika Mkutano wa Jimbo la Segerea, uliofanyika Buruguruni Sheni jijini Dar es Salaam, jana.
Diwani wa Buguruni, Busoro Pazi akieleza utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kata ya Buguruni, wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Alhaj Said Sidde akizungumza na kufungua mkutano huo.
Diwani wa Minazi Mirefu Godwin Malisa akizungumza kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Viongozi na wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwananchi akiwa ameacha kuendelea kutafuta wateja wa mito, na kuamua kusimamaili kusikiliza viongozi wakizungumza kwenye mkutano huo.
DC Mpogolo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo akiwa na Katibu wa Sisa na Uenezi mkoa wa Dar es Salaam Ali Bananga na Mbunge wa Segerea Bonna Kamoli.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omari Kumbilamoto akishusha nondo dhidi ya wapinzani wanaopotosha kuhusu uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam.
Diwani wa Kiwalani Mussa Kafana akieleza kwa kina faida za uwekezaji bandari ya Dar es Salaam, na kufuta uongo wa wapinzani kuhusu uwekezaji huo, "hawa wanaopinga na kumtusi Rais wetu Mama Samia siyo wenyewe kuna mtu nyuma yao",akasema Diwani huyo.
Mbunge wa Segerea Bonna Kamoli akieleza utekelezaji wa ilani ya CCM katikajimbo hilo.
Washiriki wakishangilia katika mkutano huo.
DC Mpogolo akimfurahia Katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Dar es Salaam Ali Bananga, wakati akizungumza  baada ya kumkaribisha jukwaani. Bamanga ameshika nafasi hiyo hivi karibuni.
Ali Bananga akizungumzia uwekezaji bandari ya Dar es Salaam, akasema, "imeshaisha hiyooo".
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala akizungumza kwenye mkutano huo.
DC Mpogolo akiendelea kuzungumza katika mkutano huo. bapmoja na masuala ya uwekezaji bandari ya Dar es Salaam, aliwataka Wananchi Buguruni hasa kina mama, vijana na wenye ulemavu kuchangankia mikopo, na pia wananchi hao wa Buguruni kujiepusha na uhalifu ikiwemo utumiaji dawa za kulevya, madanguro na wazadi kuhakikisha wanahudumia watoto wao wanaosoma hasa upande wa chakula.
Vijana wa hamasa wakimshangilia DC Mpogolo.
Wananchi wakimshangilia DC Mpogolo.

Kijana (kushoto) akimsikiliza kwa makini DC Mpogolo.Mwanamuziki wa kizazi kipya akitoa burudani mwishoni mwa mkutano huo.

MWISHO. Na Bashir Nkoromo/CCM Blog.
 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages