Mjumbe wa Halmashauri Kuuya Taifa ya CCM, Mzee Steven Wassira amewataka wananchi kuacha kuwasikiliza wapiga porojo wanaodiriki kusema kuwa bandari na nchi imeuzwa.
Amediriki kuhoji kwamba hivi nchi ikiuzwa je na sisi wananchi ni mbuzi tumeuzwa? Na kueleza kwamba wanaoeneza uongo huo ni vyama mabaraka wa mabeberu, ni kuachana nao.
Ameyasema hayo wakati wa mkutano mkubwa wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo wa kuielimisha jamii kuhusu usahihi wa makubaliano ya uendeshaji wa Bandari na Kampuni ya DP ambao baadhi wanapotosha.
Mkutano huo mkubwa umefanyika kwenye Uwanja wa Luanda, jijini Mbeya n kuhudhuriwa pia na mikoa jirani ya Iringa, Njombe, Songwe na Rukwa.
Katika mkutano huo uliohutubiwa na Chongolo, pia baadhi ya mawaziri walipata wasaa wa kuelezea usahihi huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇