Vijana waliojiunga kwa mujibu wa sheria na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakijitolea kuchangia damu katika Maonesho ya Maadhimisho ya ya Wiki ya Kilele cha miaka 60 ya Jeshi hilokwenye Viwanja vya Jengo la SUMA JKT jijini Dodoma Julai 7, 2023, ikiwa ni moja ya shamrashamra za maadhimisho hayo ambayo kilele chake itakuwa Julai 10 na mgeni rasmi atakuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais Samia Suluhu Hassani kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mkuu wa Huduma za Sheria wa JKT, Kanali Projestus Rutaiha akizungumza wakati wa uzinduzi wa uchangiaji damu kwa ajili ya wagonjwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.Kaimu Muuguzi wa Huduma za Tiba wa JKT, Meja Yusuf Sasamalo akielezea umuhimu wa uchangiaji damu na kwamba JKT nchi nzima watajitolea damu kwa muda wa siku mbili.
Mkuu wa Kitengo cha Damu Salaam wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Kucy Michael akielezea furaha kwa JKT kujitokeza mara kwa mara kuchangia damu kwa ajili ya hospitali hiyo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇