LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 30, 2023

UMOJA WA WAANDISHI WA HABARI ZA AFYA KIDIJITALI WAZINDULIWA

Mbunge Neema Lugangira (aliyekaa katikati) akiwa na  wanahabari waasisi wa Umoja wa Waandishi wa Habari za Afya Kidijitali mara baada ya kuuzindua jijini Dar es Salaam.


Na Richard Mwaikenda, Dar es Salaam


 Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Lugangira  amezindua Umoja wa Waandishi wa Habari za Afya Kidijitali 'Digital Health Journalist Group'  nchini, katika semina ya mambo ya  afya iliyofanyika  Juni 14, 2023 jijini Dar es Salaam.


Lugangira ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Agri Thamani iliyoandaa semina hiyo kwa wanahabari  kutoka mikoa mbalimbali nchini, amesema kuwa lengo la Umoja huo ni kuhabarisha Umma kuhusu mambo ya Afya.


Aidha, Lugangira amesema licha ya Umoja huo kuhabarisha Umma juu ya mambo ya Afya, jukumu lao lingine litakuwa kuchagiza mabadiliko ya kisera na sheria  ili taarifa binafsi za Afya zilindwe.


"Taarifa za Afya ni 'sensitive' na ni haki yako kuzipata, zinapaswa kulindwa, lakini tumekiwa tukiziona taarifa za wagonjwa zikisambaa hovyo mitaani na kwenye mitandao, hii siyo sahihi," amesema Lugangira.


Mbunge Lugangira amesema kuwa kuna dharula nyingi za kiafya hutokea, ikiwemo taarifa muhimu anazotakiwa mgonjwa kuzijua,kama vile grupu lake la damu, uzito na tatizo lake la kiafya, lakini wengi mambo hayo yanayowahusu hawayajui.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages