Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Kalanga Laiser akiwahutubia Wananchi wa Kata ya Nyakasimbi Wilaya Karagwe.
Na Lydia Lugakila,
KARAGWE.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera Julius Kalanga Laiser amewaagiza watendaji wa Vijijini katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani humo kuhakikisha wanawasomea Wananchi mapato na matumizi.
Hayo yamekuja baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kugundua kuwa Wananchi wamekuwa wakichangia fedha za kutekeleza miradi mingi ya maendeleo kwa juhudi kubwa huku tatizo likionekana kwa baadhi yawatendaji ambao wamekuwa hawawasomei mapato na matumizi Wananchi hao.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Kalanga Laiser wakati akihutubia Wananchi wa Kata ya Nyakasimbi katika mkutano wa hadhara.
Dc Laiser amewapongeza Wananchi kwa namna walivyopambana na kufanikisha kupata madarasa mazuri katika shule ya Msingi Nyakabila.
"Hongerani Wananchi kwa kazi mliyofanya nzuri inaonekana japo wenye pesa hawataki kusoma matumizi sasa nauliza we mtendaji inakushinda nini kusoma mapato na matumizi?" alisema Mkuu wa Wilaya hiyo.
Alisema hakuna haja kwa Watendaji kutengeneza migogoro na Wananchi badala yake wawasomee namna mapato na matumizi yalivyokwenda.
Amempongeza Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi Nyakabila kwa namna alivyosimamia ujenzi huo vyema.
Aidha amesema kuwa kwa nini mapato na matumizi yanahitajika inawezekana Kuna watu wametoa hela yao na kukuta hela hizo hazijafika Kijijini au inawezekana kukawa na Mwananchi aliyetoa mchango wake na usifike shuleni hivyo waliotoa hela na hazijafika wajulishwe na watambue kupitia kusomewa mapato na matumizi.
Aidha ameagiza Serikali ya Kijiji Kahanga Kata Nyakasimbi Wilayani Karagwe kuhakikisha ndani ya siku saba wasome mapato na matumizi
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nyakasimbi Wallence Kasumuni aliwapongeza Wananchi katani humo kutokana na kuweka nguvu kubwa katika ujenzi wa Shule hiyo kwani kwa kiasi kikubwa wamejenga kwa nguvu zao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇