Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka wazi kwamba hakitamvulia kiongozi au mtendaji yeyote atajaye kwamisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa wananchi.
Kalipio hilo limetolewa kwenye taarifa iliyosomwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Sophia Mjema baada ya kuhitimisha zaiara ya siku 7 ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo mkoani Iringa Juni Mosi, 2023.
"Kupitia ziara hizo, chama kimeendelea kuwaelekeza viongozi na watendaji wote kuwa CCM, chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan, kinatarajia watatumia dhamana zao kuleta ufanisi na matokeo yanayotarajiwa na Watanzania katika maeneo yao na kuwa CCM haitamvumilia kiongozi au mtendaji yeyote atakayekwamisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa wananchi,"amesisitiza mjema.
Aidha, kupitia ziara hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM, kuhamasisha uhai wa chama, kusikiliza na kutatua changamoto cha wananchi, ambayo ni mwendelezo wa ziara za namna hiyo anazozifanya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo katika maeneo mbalimbali nchini, chama kimeendelea kusisitiza viongozi na watendaji waliopewa dhamana mbalimbali za umma, kuwatumikia wananchi wakati wote.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇