Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni amewaonya Wananchi wanaohujumu miundombinu ya maji katika Wilayani hiyo kuacha kwani wanarudisha nyuma maendeleo.
Ametoa onyo hilo jana wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Hedaru na Mabilion ambapo amesema yoyote atakaye bainika kufanya hujuma katika miundombinu ya Miradi ya Maji ambayo inasimamiwa na (RUWASA) atachukuliwa hatua kali.
"Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pesa nyingi kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchini ili wananchi waweze kunufaika"alisema Mhe Kasilda
Aidha amemuagiza Manager Maji (RUWASA) ndugu, Abdallah Ally kuendelea kutoa Elimu kwa Wananchi pindi wanaposambaza mabomba ya maji, pia na kumtaka Diwani wa Kata ya Hedaru John Ali kuhakikisha vyazo vyote vya Maji vinatunzwa ili maji yaweze kusambazwa kwa wananchi wote wa Kata hizo mbili
Diwani wa kata ya Hedaru amempongeza Mkuu wa wilaya kwa Kazi kubwa anayoifanya kuendelea kutatua kero na migogoro kwa Wananchi wa wilaya ya Same na kuahidi kushirikiana naye kwa pamoja kwenye kuleta maendeleo katika kata ya Hedaru na Mabilion ambapo wananchi zaidi ya 5000 Katika kijiji Cha kijumo watanufaika na Mradi huo unaotekelezwa na RUWASA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇