Richard Mwaikenda
Katibu Mkuu, Daniel Chongolo amekemea tabia ya mateso na unyanyasaji wanayofanyiwa mabinti wa shule ikiwemo kuwakeketa, kuwaozesha na kuwaajiri kama wafanyakazi wa majumbani.
Chongolo ametoa onyo Hilo aliposhiriki ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa katika Shule ya Sekondari Chilonwa wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Chamwino, mkoani Dodoma.
Aidha, Chongolo ameiagiza Wizara ya Maji na Tamisemi kuandaa mpango maalumu wa kujenga miundombinu ya maji katika Shule na maeneo mengine yanayotoa huduma za jamii nchini.
Katika ziara hiyo yenye lengo la kakagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya nwaka 2020-2925, kuhamasisha uhai wa chama kuanzia ngazi ya Shina na kusikiliza kero za Wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇