Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akipokea taarifa ya mradi wa maji wa Handali uliopo Jimbo la Mvumi, wilayani Chamwino alioukagua na kuagiza uwe umekamilika ndani ya miezi miwili na nusu ili wananchi waanze kupata maji badala kila mara kuoneshwa kwenye ramani.
Mradi huo ambao umekwama kukamilika kwa wakati unagharimu zaidi ya sh. mil. 600 na ukikamilika utahudumia zaidi ya watu 8000.
Chongolo ametoa agizo hilo kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Dodoma wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo.
Katika ziara hiyo yenye lengo la kakagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya nwaka 2020-2925, kuhamasisha uhai wa chama kuanzia ngazi ya Shina na kusikiliza kero za Wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni, Issa Haji Gavu.
Chongolo akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Mvumi, Livingstone Lusinde.
Chongolo akihutubia na kutoa agizo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Gift Msuya akiteta jambo na Lusinde.
IMEANDALIWA NA RIDHARD MWAIKENDA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇