LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 2, 2023

WAZIRI MKUU, SPIKA WAFURAHISHWA NA MAZIWA YA ASAS+video

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson wamefurahishwa na bidhaa za maziwa walipotembelea Banda la Kampuni ya ASAS katika Maonesho ya Wafugaji na Wavuvi yaliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 2, 2023.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dkt. Tulia Ackson wamefurahishwa na bidhaa za maziwa walipotembelea Banda la Kampuni ya ASAS katika Maonesho ya Wafugaji na Wavuvi yaliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Aprili 2, 2023.
Walipoofika katika banda hilo walifurahi pia kukutana na mabalozi wa kampuni ya ASAS, Walipokutana na mchekeshaji maarufu Lucas Mhuvile 'JOTI' na Salama Jabir. Kama kawaida yake JOTI alifanya vituko vyake kiasi cha kuwafanya viongozi hao kuangua vicheko.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipatiwa zawadi ya maziwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ASAS, Fuad Asas baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo.
Waziri Mkuu akiangalia moja ya bidhaa za maziwa .
Waziri Mkuu akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa aina mbalimbali za bidhaa za maziwa.
Mchekeshaji maarufu, JOTI akifanya vituko mbele ya Waziri Mkuu.
Spika wa Bunge, Dkt.  Tulia akipokea zawadi kutoka kwa mchekeshaji JOTI baada ya kutembelea Banda la Asas.
Dkt. Tulia akipata maelezo alipotembelea banda hilo.


 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video, Majaliwa na Dkt Tulia wakiwa katika banda hilo...

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages