LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 23, 2023

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA MABALOZI WANANE

Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa mabalozi wanane wakiwamo maofisa wawili kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa.

Taarifa iliyotolewa leo Mei 22, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus imesema uteuzi huo ulianza Mei 10, 2023. Walioteuliwa ni pamoja na Meja Jenerali Ramson Mwaisaka, kabla ya uteuzi huo alikuwa mkuu Kamandi ya Jeshi la Wanamaji.

Wengine ni Meja Jenerali Paul Simuli aliyekuwa Mkuu wa Utumishi wa Jeshini, pia yumo Mohamed Awesu ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Konseli Mkuu, Konseli ya Jeddah Saudi Arabia.

Taarifa imesema wengine ni Dk. Mohamed Juma Abdallah, kabla ya uteuzi huo alikuwa katibu tawala wa mkoa wa Kaskazini Unguja, Hassan Mwamweta ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Ofisa mwandamizi wa Mambo ya Nje na Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania, Uturuki.

Mbali na hao mkuu huyo wa nchi, amewateua Iman Njalikai ambaye kabla ya uteuzi alikuwa Ofisa wa Mambo ya Nje Mkuu na Msaidizi wa Waziri Mkuu Hotuba na Khamis Mussa Omar ambaye alikuwa Kaimu Mwakilishi wa Kudumu, Ubalozi wa Tanzania Ufaransa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Ikulu, mabalozi hao wataapishwa kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kazini.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages