LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 6, 2023

NAIBU WAZIRI KIRUSWA AAMURU BICON ZIWEKWE KWENYE MIPAKA YA WAWEKEZAJI WA MADINI





 Naibu Waziri wa Madini Dk.Steven Kiruswa ametoa wiki moja kuweka alama (bicon) kwenye mipaka baina ya wawekazaji wawili wa uchimbaji wa madini aina ya Gypsum kati ya Kitivo Investment na Digalla Company ili kuepusha migogoro ya uchimbaji wa madini katika eneo hilo.


Ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara mkoani Kilimanjaro katika wilaya ya Same Kata ya Makanya wakati akisuluhisha mgogoro kati ya m
wekezaji wa kampuni ya Kitivo na Mwekezaji Digalla.

Mwekezaji wa Kitivo anamlalamikia mwenzie wa Digalla kumuingilia katika eneo lake la uchimbaji wa Madini ya Gypsum na hivyo anataka kampuni ya Digalla kumlipa fidia kutokana na kuchimba Gypsum kwenye eneo lake.

Kwa upande wake mwekezaji wa kampuni ya Digalla amekiri kuingia kwenye eneo la mwenzie bila kujua kutokana na kutokuwepo kwa alama za mipaka ambapo ameahidi kumpa sehemu ya kipande ambayo bado haijachimbwa kutoka kwenye eneo lake kama fidia.

Baada ya suluhisho hilo mwekezaji wa Kitivo Investment amekubali fidia hiyo kutoka Kampuni ya Digalla.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Same Mhe Kasilda Mgeni amewataka wawekazaji hao kushirikiana kwa pamoja katika kujenga Uchumi wa Taifa letu na wachimbaji wengine wote kuzifanyia ukarabati barabara ambazo Maroli yao yanapita hili Wananchi wasipate tabu kupita kufata huduma za kijamii 

Mbalimbali na hayo yote Afisa Madini Mkoa kilimanjaro Fatma kyondo amewasisitizia wachimbaji hao kuzingatia kanuni na sheria za uchimbaji wa Madini. Nakuakikisha wanafukia mashimo kwa haraka maeneo ambayo yamechimbwa Mawe hayo ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea, na yeyote asiyewajibika kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake"alisema Kyondo

Pamoja na hayo yote Naibu Waziri wa Madini,Kiruswa amemugiza Afisa wa Madini Mkoa Kilimanjaro Fatma Kyondo kuwasimamia wawekezani hao wakati wakikabidhiana fidia iliyoahidiwa ili kumaliza mgogoro huo.

Wawekazaji hao wameshukuru ujio wa Naibu Waziri na kuweza kutatua Mgogoro huo na wameahidi kutotokea tena mgogoro baina yao.

Aidha wameahidi kuweka alama za mipaka (bicon) kama walivyoelekezwa ili kuendelea kukuza Uchumi wa nchi ambapo pia wamemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuamini wachimbaji wadogo wa Madini ya Gypsum.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages