LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 14, 2023

DC KILOMBERO AFUTA TANGAZO TATA LA MKURUGENZI WA MLIMBA BAADA YA AGIZO LA UONGOZI WA CCM WILAYA KILOMBERO


 Na Dismas LYASSA

WANANCHI wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba wamempongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kilombero, ndugu Mohammed Msuya kwa kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa Ilani ikiwamo kuzuia waziwazi mpango wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlimba kumtaka kila mwananchi anapovuna mazao shambani mwake kwa ajili ya kuuza au chakula awe analipa ushuru wa Tsh1000 kwa gunia.


Wananchi pia wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Dunstan Kyobya ambaye nae ametangaza kulifuta tangazo hilo kufuatia wananchi kila maeneo katika halmashauri hiyo kulalamikia uamuzi huo ulionekana kama ni tata kwao.  


Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo la wananchi kutakiwa kulipia Tsh1000 kwa gunia, Mkuu hiuyo wa alijibu "Nimeshalifuta hilo".

Wiki iliyopita ofisi ya Mkurugenzi wa Mlimba ilitoa maagizo ikiwataka maofisa watendaji katika katika vijiji na kata zote katika Halmashauri hiyo kuhakikisha wanafuatilia mapato ikiwamo kuhakikisha kila gunia la mazao linatozwa Tsh1000 hata kama linatolewa shambani kuletwa nyumbani kwa mkulima kwa matumizi ya chakula.


Agizo hilo lilileta malalamiko mengi kwa wananchi, jambo lililosababisha Mwenyekiti huyo wa CCM kuitisha kikao cha dharura cha chama na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Mlimba akiwamo Mkurugenzi na madiwani wake waliopitisha tuzo hiyo.


Katika mkutano huo madiwani walisema suala hilo lilipitishwa kwenye kikao chao cha Oktoba mwaka jana na kwamba walikubaliana baadae wangewasilisha mpango huo kwenye chama, kitu ambacho hawakufanya, badala yake wamelipeleka moja kwa moja kwa wananchi kwa utekelezaji bila hata kuwa na mikutano na wananchi.


“Mpango huo hauna baraka kutoka kwa chama wala wananchi, nazuia usiendelee,” alisema Msuya, huku baadhi ya madiwani wakishindwa kufafanua hasa namna gani walipitisha mpango kama huo.


Wananchi wamekipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa kusimamia Serikali na kujali wananchi, huku baadhi yao wakiomba ofisi ya waziri mkuu kuangalia upya ofisi ya Mkurugenzi inavyofanya shughuli zake na namna inavyoshirikiana na baadhi ya madiwani katika kuendesha mambo yake bila ridhaa ya chama tawala wala wananchi.


Mwenyekiti wa chama ameongeza hatokubali kuona serikali inayoongozwa na Mh Rais mama Samia Suluhu Hassan wananchi wake wateseke wakati wana imani na mh Rais kwa kazi nzuri anayoifanya kuwaletea maendeleo jimbo la Mlimba

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages