LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 17, 2023

BILIONI 20 KUMTUA MAMA MAJI KICHWANI JIMBO LA BUKENE

Mbuge wa Jimbo la Bukene akizungumza juu mradi mkubwa wa MAJI kwenda jimboni kwake kwenye sherehe za wiki ya Wazazi CCM kutumiza miaka 67.Picha na Odace RWIMO

Na Odace Rwimo Nzega

Mbunge wa Jimbo la Bukene Wilayani Nzega Seleman Zedi amebainisha kuwa serikali ya awamu ya sita imewekeza nguvu kubwa katika kutatua shida ya MAJI jimboni jumo

Akinzungumza katika wiki ya Jumuiya ya  wazazi Wilayani Nzega iliyofanyika kata ya Shigamba aliwambia wanachama wa CCM kuwa tayari mradi wa kupeeka MAJI jimboni hapo umeisha Anza.

Alisema mradi huo utagharimu BILIONI 20 ambapo kwa mwaka fedha 2022/2023 tayari wamwpokea kiasi Cha BILIONI 5 ili kuanza kutekeleza mradi huo makubwa.

Zed alimpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa mapenzi yake ya Dhati aliyoyaonesha katika kuwajali wananchi wa Jimbo la Bukene kwa kuwapelwkea MAJI ya ziwa Victoria Jambo ambalo limekuwa no furaha kwa Kila mwananchi.

Alisema Jimbo Hilo limekuwa likikabiliwa na ukosefu wa MAJI ya kujitosheleza kwa baadhi ya kata Hali iliyochangia wananchi kupata shida na adha kubwa ya kufuata MAJI mwendo mrefu na wakati mwingine kuhatarisha maisha yao.

Mkuu waWilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bukene Selemani Zedi pamoja na baadhi ya viongozi Wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Nzega wakikagua miradi ya Maendeleo kwenye wiki ya Wazazi

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM  Wilayani Nzega Ashura Ngade alisema wanajivuni
Mafanikio ambayo yanayotokana mipango dhabiti na utawala Bora Chama Cha Mapinduzi.

Alisema kwenye Chama hiki Jumuiya ya Wazazi ndio kubwa kwani Sasa tunaadhimisha kutumizi miaka 67 Jambo ambalo ni kubwa kwetu ambapo tunazidi kusimamia Elimu na malezi Bora  kwa kiwango kikubwa.

Alisema mafanikio ya CCM pia Kuna mchango wetu makubwa hasa katika kusimamia na kutekeleza majukumu yetu Kama Jumuiya longer na yenye historian kubwa ndani ya Chama hivyo tutaendelea kumuunga mkono Rais wetu mpendwa kwa Kila kitu anachokifanya ndani ya serikali na Chama kwa ujimla.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai alisema Jumuiya ya Wazazi inao wajibu makubwa wa kuendelea kutunza na kulinda maadili ya taifa Hili kwani ni moja ya jukumunlao kubwa.

Alisema Jumuiya hiyo kwa Sasa ndio wakati mwafaka wa kupambana na Hali ya kuporomoka kwa maadili kwa Kasi ikiwa ni pamoja kukemea Ushoga ambao limekuwa ni janga la dunia kwa sasa.

Alisema ili kuweza kufikia malengo ambayo yatakuwa na tija kwa taifa Jumuiya hiyo inapaswa kuanzishwa makongamona ya mashuleni na hata mikutano ya Hadhara ya kuikibusha jamii kutunza tumaduni zao na kulinda haki za watoto kwa ujimla.

"Ili tuweze kulinda kizazi chetu Kuna haha kubwa ya kuweza Sasa kuwalinda vizazi vyetu kwani Hali ya dunia ni mbaya hivyo no wajibu wetu Kama wazazi kushikamana ni kukemea maovu yanayoonekana kuharibu watoto wetu"alisema Tukai

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages