LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 17, 2023

BILIONI 1.869 KUJENGA KILOMETA 2.8 KIWANGO CHA RAMI NZEGA

Mhandisi Sumbuko Twaha akiwaelekeza Jambo mafundi ambao wanajenga Matulo kwenye Barabara Mpya ya Rami wakati alipotembelea hapo kuona Maendeleo ya ujenzi huo

 Na Odace Rwimo, Nzega

Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini Nchini, TARURA Wilayani Nzega Mkoani Tabora katika kuendelea kuboresha mji wa Nzega wamekamilisha Barabara ya kiwango Cha yenye urefu wa KILOMETA 1.5.

Akizungumza na vyombo vya habari Meneja wa TARURA wilayani hapo Haruna Mbagalla alisema kwa mwaka huu wa fedha kutoka mfuko maalumu wamepanga kujenga Zaid ya KILOMETA mbili za Rami huku kilometa 1.5 zikiwa asilimia 98 kukamilika.

Alisema kipenda hicho Cha rami kitakapo kamilika kitafungwa taa ili kufanya mji kuwa wa kisasa na muonekano wa kuvutia ikiwa ni hatua ya kuendelea kuboresha miundombinu ya Barabara za mjini kwa kiwango Cha rami.

Alisema licha ya ujenzi wa Barabara kwa kiwango Cha rami lakini wanaendelea na ufunguzi wa Barabara maeneo mengine ya wilaya ya Nzega ambayo yalikuwa hayapitiki kwa kipindi chote.

Mhandisi Sumbuko Twaha akionesha Daraja kubwa liloogharimu takaribani milioni 350 katika barabara ya Nzega- Igilali- Idudumo. 

Mbagalla alisema TARURA Wilaya wanaendelea na ujenzi wa madaraja makubwa ambapo hivi Sasa wamekamilisha zaidi ya Marsha yenye zaidi thamini ya milioni 900 kwenye maeneo yaliyokuwa Yana uhitaji mkubwa wa madaraja huku wakiendelea na ujenzi wa miataro maeneo yote ya Barabara za mji.

Hata hivyo alisema wapo kwenye mpango wa uwekaji wa Taa za barabarani 25 katika Barabara za mji wa Nzega ambazo zitagharimu milioni 75 ambapo uwekaji huo utafanya mji kuwa na Hali ya kuvutia maeneo yote ya mji na muonekano wa kipekeee wakati wote wa usiku.

Kwa upande wake mhandisi SumbukoTwaha alisema mpango wa bajeti wa mwaka 2023/2024 katika wilaya ya Nzega unaelezea mafanikio makubwa waliyopata kwenye utawala wa awamu ya sita.

Alisema katika mpango huo wilaya ya Nzega inakadiria kutumia zaidi ya bilioni 8 kufanya matengenezo na kufungua Barabara ,kujenga makaravati,kujenga madaraja,kuweka Taa za barabarani ikiwa ni pamoja kujenga Barabara za Rami maeneo mbalimbali ya mji wa Nzega.

"Ukiangalia kwenye bajeti yetu ambayo tunaendelea kuitekeleza utaona maeneo mengi ambayo tumefungua Barabara mfano mzuri Kata ya Mizibaziba -Kipugulu-Mwisi hii no Barabara mpya kabisaa ambayo imegharimu zaidi ya milioni 76" alisema Mhandisi Twaha.

Alieleza kuwa Kuna Barabara ya Mwangoye - Sigili hii pia tumeifanyia matengenezo maalumu zaidi kilometa 15 ambayo imegharimu zaidi ya milioni 147 hivyo kufanya kata hizi mbili Sasa kuwa na mtandao wa Barabara inauoziunganisha Jambo ambalo kabla halikuwepo.

Muonekano wa Barabara ya Rami inayoendelea kujengwa mjini Nzega kwa fedha maalumu.

Hata hivyo alisema Kuna licha ya Taa 25 za awali katika mji wa Nzega tunaendelea na mpango mwingine wa uwekaji wa Taa 75 ambapo zitagharimi zaidi ya Milioni 220 hivyo kufanya mji kuwa na Taa karibia 100 zitakazo kuwa maeneo ya mji wa Nzega.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages