LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 2, 2023

BALOZI WA MAREKANI AJITAMBULISHA KWA RAIS DK. MWINYI, IKULU ZANZIBAR, LEO

Ikulu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi  amesisitiza kuwa Serikali inaunga mkono uwekezaji katika maeneo ya uchumi wa Buluu ikiwemo usafirishaji wa Baharini, mafuta, gesi na Bandari. 


Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo kumweleza Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Michael Anthony Battle ambaye alimtembelea kujitambulisha, Ikulu mjini Zanzibar, leo.


Dk. Mwinyi amesema, kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kumetokana na makubaliano yaliyofanyika baada ya uchaguzi ili kutafuta njia za kutatua tofauti zilizopo na kushirikiana kuendesha na kudumisha amani na utulivu nchini. 


Naye, Balozi wa huyo alieleza  kuridhishwa na utendaji wa Rais Dk. Mwinyi kwa utayari wake katika sekta ya biashara na uwekezaji ikizingatiwa kuwa Marekani imelenga kuwekeza zaidi nchini na kutoa fursa za ajira.

Rais Dk. Hussein Mwinyi akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Michael Anthony Battle ambaye alimtembelea kujitambulisha, Ikulu mjini Zanzibar, leo.

Rais Dk. Hussein Mwinyi akizungumza na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dk. Michael Anthony Battle ambaye alimtembelea kujitambulisha, Ikulu mjini Zanzibar, leo.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages