LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 19, 2023

AIRTEL YANG’AA MAONESHO YA WADAU WA MAWASILIANO VIWANJA VYA BUNGE DODOMA





Kampuni ya Simu ya mkononi ya Airtel leo imeendelea na maonesho ya baadhi ya Huduma na bidhaa wanazotoa ambapo waheshimiwa wabunge na viongoz mbali mbali wamejitokeza kwa Lengo la kupata huduma zao.

Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Akson aliingoza wabunge wengine leo kupata Huduma kutoka kwa wadau wa Mawasiliano ambapo pia alitembelea banda la Airtel viwanjani hapo.

Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alimkaribisha Spika na kumpatia ZAWADI Maalum ya Rauter ya Intanet inayoweza kuunganisha watu zaidi ya 32 kwa Wakati mmoja na Kisha kumweleza mheshimiwa Spika kuwa Airtel inamkabidhi zawadi kwa kuwa inajiamini sasa hata akiwa mkoani (Jimboni) ataunganishwa na Intaneti ye ye Kazi kwa kuwa asilimia 90 ya Minara ya Airtel sasa imeunganishwa teknolojia ya 4G ikiwemo minara ya mbeya.


Maonesho ya wadau wa mawasiliano yanaendelea kwa siku 3 katika viwanja vya bunge ikiwa ni kuelekea kwenye bunge la bajeti ya Mawasiliano linalotarajiwa kusomwa kesho na Waziri wa Habari na Mawasiliano Mheshimiwa Nape Mnauye.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages