LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 23, 2023

ZIARA YA KOMREDI CHONGOLO NCHINI CHINA

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameendelea na ziara kikazi nchini China huku akiongozana na viongozi wengine wa CCM, wakiwemo Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC, Wenyeviti wa Mkoa pamoja na Wenyeviti wa Jumuiya.

Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM inalengo la kuendeleza mahusiano ya Kirafiki na Kindugu yaliyopo kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Kikomonisti Cha China (CPC).

Pamoja na Mambo Mengine CCM na CPC zimejikita zaidi katika kusaidiana katika mambo ya Elimu na Mafunzo ya Falsafa ya Siasa na Uchumi. Mahusiano kati ya vyama hivi, yameasisiwa na waanzilishi wa vyama hivyo vikongwe na kuendelea kuimarishwa na viongozi wa sasa.

Ziara hii imeanza tarehe 16 Aprili, 2023 na inatarajiwa kumalizika tarehe 26 Aprili, 2023.



 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages