LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 2, 2023

YANGA SC YAWAPIGA TP MAZEMBE 1-0 NA PALE PALE LUBUMBASHI


BAO pekee la Farid Mussa dakika ya 63 limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, TP Mazembe katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Yanga SC inamaliza na pointi 13, ikiendelea kuongoza mbele ya Monastir ya Tunisia yenye pointi 10 ambayo baadaye usiku itamenyana na Real Bamako Jijini Tunis.

Kama Monastir watashinda kwa wastani wa zaidi ya mabao matatu basi wataongoza kundi hilo dhidi ya wana Robo Fainali wenzao, Yanga SC.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages