MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa (kulia) akimkabidhi Afisa Habari wa Yanga SC, Ally Kamwe fedha taslimu Sh. Milioni 10 zawadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mabao yao mawili waliyofunga kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Rivers United Jumapili nchini Nigeria.
Ilikuwa mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na timu hizo zitarudiana Jumapili ya wiki hii Uwanja wa BenjamĂn Mkapa Jijini Dar es Salaam, Yanga ikihitaji sare tu kwenda Nusu Fainali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇