MLATA AMPONGEZA RAIS DK. SAMIA
Na HEMEDI MUNGA
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Singida, Martha Mlata amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea
kutekeleza Ilani ya chama hicho katika sekta ya michezo.
Mlata anamshukuru Rais Dk. Samia kwa kuhamasisha
michezo kwa kutoa fedha kuzipatia timu za Simba, Yanga na Taifa Stars katika
kila goli wanalofunga katika michuano ya kimataifa inayoshiriki timu hizo.
Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari punde baada ya kukagua uwanja wa Liti mkoni
hapo baada ya kiwanja hicho kuchaguliwa kutumika katika michuano ya Shirikisho la
Azam Federation Cup Nusu Fainali,
Mwenyekiti huyo anasema Rais Dk. Samia katoa fedha kwa wanamichezo kwa lengo la
kuendelea kutekeleza resa za chama hicho katika michezo.
‘’Tunamshukuru sana Rais DK. Samia hakika yeye ni
mdau mkubwa sana wa michezo,’’ anashukuru.
Aidha, anasema kutokana na fursa hizo na nyingine,
wao wanahamasisha michezo shuleni kwa lengo la kuhakikisha wanaendelea kuibua
vipaji, waliyo na vipaji kuwaunganisha na fursa mbalimbali.
Kuelekea michuano hiyo ya nusu fainali ya kombe la
Azam Federationi Cup, Mwenyekiti huyo anasema ujio wa timu hizo ni fursa kwa
wananchi wa mkoa huo kwa sababu watafanya biashara mbalimbali.
‘’Tumepokea kwa furaha sana kuwa uwanja wetu
kuteuliwa kuwa moja ya viwanja
vitakavyochezewa nusu fainali ya michuano ya Shirikisho la Azam
Federation Cup,’’ anashukuru.
Aidha, Mlata analishukuru Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kwa kulichagua dimba la Liti litumike katika michuano hiyo.
‘’Hakika tunafahamu viwanja vipo vingi ambavyo ni
vizuri lakini TFF wameuchugua uwanja wetu wa Liti, tunawashukuru sana,’’
Kutokana na ofa hiyo, Mlata anamshukuru Meneja wa
uwanja huo kwa sababu ameendelea kuutunza hasa namna pichi yake inavyoonekana
katika sura nzuri.
Anasema hakika Meneja huyo anafanya kazi nzuri sana
ambayo imewezesha TFF kuuchagua uwanja huo, hivyo amefanikiwa kuupa sifa mkoa
huo.
‘’ Kwa kweli wananendelea kutupa raha, sifa na heshima
kwa sababu kazi anayoifanya Meneja inaonekana na ndio maana TFF wameuchugua,’’ anasema.
Halikadhalika, anasema ni fursa kwa wajasiriamali na
wafanyabiashara wa mkoa huo kufanya biashara ikiwemo katika nyumba za kulala
wageni.
Anasema mkoa huo una malighafi nyingi zikiwemo mahindi,
karanga, asali, vitunguu, kuku wa kienyeji, mayai na mafuta ya alizeti.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Soka
mkoa wa Singida amabye ni Diwani wa kata ya Kindai (SIREFA), Omary Hamisi anasema
itakuwa ni heshima kwa mkoa huo kama timu ya Singida Big Star itaingia nusu fainali
ya michuano hiyo.
Aidha, anawahakikishia wapenzi na washabiki wa soka
Tanzania kuwa timu yao itasonga mbele katika michuano hiyo.
Michuano ya kome la Shirikisho la Azam Federation
Cup inatarajia kitimua vumbi April 7 na 8 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Singida, Martha Mlata akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari punde baada ya kukagua uwanja wa Liti mkoa wa
Singida baada ya kiwanja hicho kuchaguliwa kutumika katika michuano ya Shirikisho
la Azam Federation Cup Nusu Fainali.(Picha
kwa hisani ya ofisi ya chama)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Singida, Martha Mlata akikagua uwanja wa Liti. (Picha kwa hisani ya ofisi ya
chama)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Singida, Martha Mlata akikagua pichi ya uwanja wa Liti. (Picha kwa hisani ya
ofisi ya chama)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇