LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 9, 2023

KICHEKO ZANZIBAR, BEI ZA PETROLI NA DISELI ZASHUKA, YA NDEGE YASHUKA ZAIDI

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei za mafuta Visiwani humo kwa mwezi huu wa Aprili 2023, ikionyesha neema kuwa kubwa zaidi kwa wamiliki wa vyombo vya moto.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo jana, Aprili 8, 2023 imesema, huwa inapanga bei kwa kuzingatia wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta duniani, gharama za uingzaji katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.

Pia Mamlaka hiyo inazingatia, thamani ya shilingi ya Tanzania na Dola ya Kimarekani, gharama za usafiri, bima na premium hadi Zanzibar, Kodi na tozo za Serikali ikiwemo kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

ZURA imesema, bei za mafuta kwa mwezi huu wa Aprili 2023, Lita ya Petroli itauzwa kwa sh. 2,780 tofauti na bei ya mwezi mwezi uliopita wa Machi, ambao ilikuwa sh. 2. 880 kwa lita, na Dizeli kwa mwezi huu Aprili 2023 lita inauzwa sh. 2,900 tofauti na mwezi Machi ambao lita ilikuwa sh. 2023.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ZURA mafuta ya taa kwa mwezi huu wa Aprili  2023 haikupanda wala kushuka kwa kuwa lita inauzwa sh. 2,021 sawa na bei ya mwezi uliopita wa Machi ambao lita moja ilikuwa inauzwa kwa bei hiyo hiyo ya sh, 2, 921.

Wakati hali ikiwa hivyo kwenye Petroli, Dizeli na mafuta ya taa neema kubwa imeonekana kwenye mafuta ya Ndege ambayo mwezi huu bei yake imeshuka kutoka bei ya sh. 2,681 ya mwezi uliopita wa Machi hadi kuuzwa kwa 2,500 mwezi huu wa  Aprili 2023.

ZURA imesisitiza katika taarifa yake kuwa itaendelea kufuatilia na kudhibiti soko la mafuta na bei zake  kwa karibu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha  bei za bidhaa hizo haziongezeki mara dufu na kusababsha athari katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi.
 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages