LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 8, 2023

KAA CHONJO, MAJIZI YATUMIA BARUAPEPE FEKI YA IKULU KUTAPELI WATU WATOE PESA ILI WATEULIWE AU WAPATE AJIRA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Ofisi ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema kuna baadhi ya Watu wamekuwa wakitumia Ofisi hiyo na jina la Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus kwa baruapepe ya zuhuranus250@gmail.com kutapeli kuwa wanaweza kuwaunganisha kupata teuzi mbalimbali na nafasi za kazi.

Mkurugenzi huyo Zuhua Yunus, ametoa taarifa kuwawatahadharisha watu kuwa macho ili kuwaepuka matapeli hao hatari.

"Aidha watu hao kupitia baruapepe hiyo (zuhurayunus250@gmail.com), wamekuwa wakiomba watu kutuma kiasi cha fdha ili wapate nafasi za uteuzi katika taasisi mbalimbali za Serikali.

Napenda kuwataarifu kuwa, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu haihusiki na baruapepe hiyo au maamuzi yoyote ya Uteuzi.

Hivyo epukeni kutapeliwa, mnapopokea ujumbe kutoka kwa watu hao", imesema sehemu ya taarifa ya Zuhura Yunus (pichan).


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages