LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 2, 2023

ROUTE MPYA ZA DALADALA ZAZUA MKANGANYIKO DODOMA, RC SENYAMULE ALONGA+video

Mabadiliko ya njia za daladala Dodoma yamesababisha mkanganyiko hasa baada ya kituo maarufu cha soko la Sabasaba kufungwa na kuelekeza daladala kuanzia sasa kubeba na kushusha abiria itakuwa Soko jipya la Machinga Complex. Mabadiliko hayo yamelalamikiwa na baadhi ya wananchi na wafanyabiashara kama wanavyojieleza walipohojiwa na mwandishi wetu eneo la Sabsaba Machi Mosi, 2023... Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rose Senyamule ametoa neno kuhusu mabadiliko hayo alipokuwa akihutubia wakati wa uzinduzi wa kituo cha daladala katika soko la Machinga Complex.



Kifusi kikiwa kimewekwa eneo la sabasaba  ambapo kituo cha daladala kimeondolewa.
Wananchi wakitembea kutafuta vituo vya kwenda kwao baada ya kituo cha sabasaba kuhamishwa.


Daladala zikiwa zimeegeshwa katika kituo kipya cha Machinga Complex jijini Dodoma.


PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, baadhi ya wananchi wakielezea kuhusu mkanganyiko huo huku Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Senyamule akitoa neno....

 

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages