Na CCM Blog Arusha
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ametoa mwito kwa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) kutumia nguvu ya Chama chao kuungana na kila chama cha siasa kumkomboa mwanamke wa Tanzania.
Rais Samia amesema hayo wakati akihutubia katika Kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lilioandaliwa na BAWACHA katika Ukumbi wa Kuringe.
Aidha, Rais Samia amesema lengo ni kuona mwanamke wa kitanzania anathaminiwa na kupewa haki kama mwingine yeyote duniani kwa kuwa changamoto hazichagui dini, kabila wala itikadi ya kisiasa.
Rais Samia pia amewataka wanawake kutumia siku hii kutathmini maendeleo ya wanawake na changamoto wanazokabiliana nazo kisiasa, kiuchumi na kijamii ili kupata maridhiano ya haki zao katika usawa wa kijinsia.
Vile vile, Rais Samia amevitaka vyama vya siasa kufanya kazi kwa pamoja na kushikamana ili kukuza siasa za kistaarabu na za kusikilizana zitakazoleta heshima kwa taifa na kustawisha uchumi.
Rais Samia pia amesema alitumia ubunifu kuunganisha taifa kwa kuhakikisha kunakuwa na maridhiano na uvumilivu.
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi mbalimbali wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), na Wanachama wa Chama hicho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023.
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Maridhiano kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA Freeman Mbowe, aliyeikabidhi kwa niaba ya Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) baada ya kuwahutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023.



No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇