LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 22, 2023

MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR DK. MWINYI AMLILIA MUASISI WA UMOJA WA WANAWAKE WA AFRO-SHIRAZ PATRY ASYA AMOUR

Na Is-haka Omar, Zanzibar
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Chama kimepata pigo kubwa kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa mwanzo wa Umoja wa Wanawake wa Afro-shirazi Party (ASP), Bi. Asya Amour, kilichotokea Machi 19, mwaka 2023 nyumbani kwake Bububu Unguja.

Dk. Mwinyi amesema CCM imepata pigo kwa kuwa Bi. Asya Amour  alikuwa muasisi mahiri, mzalendo, mchapakazi, mwanamapinduzi na mwanaharakati mbobezi wa haki za wanawake Tanzania.

“Marehemu Bi. Asya ni miongoni mwa wanawake wa mwanzo waliokuwa mstari wa mbele kutetea,kulinda na kusimamia maslahi ya Chama Cha Afro-shira Party,alijitolea bila hofu kusimamia haki za wanawake daima tutamkumbuka na kuenzi maono na falsafa zake kwa vitendo”,. Amesema Dk. Mwinyi.

Kada huyo Bi. Asya Amour amezaliwa mwaka 1928, kijijini kwao Bwejuu Wilaya ya Kusini Unguja,enzi za uhai wake ameshika na kutumikia nyadhifa mbalimbali ndani ya Chama na Serikali tokea ASP,na CCM zikiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha ASP.

Wadhifa mwingine aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya watu 20 walioteuliwa kutayarisha Katiba ya CCM ya mwaka 1977,mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM Taifa pamoja na Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chama Cha Mapinduzi kinawaomba wawe na subira na ustahamilivu ndugu,jamaa,marafiki,wanachama na makada wa CCM nchini katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Marehemu Bi. Asya Amour amezikwa Jumatatu Machi 20,mwaka 2023 katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Mkoa wa Mjini na Magharibi Unguja.

Aidha Chama Cha Mapinduzi katika mazishi ya kada huyo na muasisi kimewakilishwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Khadija Salum Ali. Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

Rais Dk. Mwinyi

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages