LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 14, 2023

MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI KUJA TANZANIA MWISHONI MWA MWEZI HUU

Na Bashir Nkotomo, CCM Blog

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harri, atafanya ziara ya wiki moja Barani Afrika ambapo atakuwa nchini Tanzania kuanzia Machi 29 hadi 31. 


Taarifa zimesema, katika ziara hiyo ataanzia Ghana, Machi 26 hadi 29, kisha ndipo atakuja Tanzania kuanzia Machi 29 hadi 31 na kituo chake cha mwisho kitakuwa Zambia Machi 31 na Aprili mosi


Duru za Siasa zimesema Makamu huyo wa Rais pamoja a mambo mengine, anafanya ziara hiyo Afrika kwa lengo la Marekani kuongeza mawasiliano yake kwa bara hilo huku kukiwa na ushindani wa Kimataifa, haswa na China.


"Safari hii itaimarisha ushirikiano wa Marekani kote barani Afrika na kuendeleza juhudi zetu za pamoja kuhusu usalama na ustawi wa kiuchumi", ilisema taarifa kutoka kwa Kirsten Allen ambaye ni msemaji wa Makamu wa wa Rais.


No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages