Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, wametakiwa kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kila mara ili kuimarisha afya ya mwili na akili ili kuwawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Raslimali Watu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi, Prisca Lwangili Jijini Dodoma alipoongoza program ya mazoezi ya kila siku ya Alhamisi kwa watumishi wa Wizara hiyo leo jioni.
Bi. Lwangili, amefafanua kuwa lengo la program hiyo ni kuwapa fursa wa Watumishi wa Wizara hiyo kufanya Mazoezi kama mkakati wa kuongeza ufanisi kazini Kwa kuwajengea afya njema ikiwa ni pamoja na kujenga mshikamano na upendo kazini baina yao
Aidha, Bi. Lwangili ametoa wito kwa Watumishi wa Wizara hiyo pamoja na Taasisi zake ambazo zipo katika Mikoa mingine kuazisha program ya Mazoezi kwenye maeneo yao ili kila mtumishi wa Wizara hiyo apate nafasi ya kufanya mazoezi.




No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇