Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Komredi Abdulrahman Kinana akihutubia alipokuwa akifungua mafunzo ya wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja Wanawake Tanzania (UWT TAIFA) kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Machi 21, 2023.
Kinana amesema kuwa UWT ni nguzo kuu ya chama hicho, wanaiamini na kuitegemea.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda akimpatia tuzo maalumu Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana kwa kutambua mchango wake katika chama.
Chatanda akihutubia kabla ya kumkaribisha Komredi Kinana kufungua mafunzo hayo.Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Wanawake, Jinsia na Makundi Maalumu, Dkt. Doroth Gwajima akitoa mada kuhusu mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT wakiimba wimbo wa hamasa wakati mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Philis Nyimbi akitoa utambulisho kwa wajumbe.
Komredi Kinana akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa, Zainab Nassoro.
Waziri wa Nishati, January Makamba akiwasilisha mada kuhusu nishati safi ya kupikia ambapo aliahidi serikali kugawa majiko ya gesi katika ofisi za UWT nchini kwa ajili ya viongozi kutolea mafunzo kwa wanawake kuhusu umuhimu wa kutumia majiko hayo badala ya kuni au mkaa.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Kinana akielezea umuhimu huo wa UWT.....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇