LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 14, 2023

KINANA AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI NA WA MISRI, WA MAREKANI AMSIFU RAIS SAMIA KUIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI

Machi 14, 2023
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amekutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Marekani na  Balozi wa Misri, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Kinana akizungumza na Balozi wa Marekani Michael Battle, wote wamegusia kuimarisha Ushirikiano katika nyanja mbalimbali baina ya Tanzania na Marekani.

Kwa upande wake Balozi wa Marekani  ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna inavyoendelea kupiga hatua katika kuimarisha Demokrasia, Utawala wa Sheria, Uhuru wa Kisiasa na Utawala bora.

Aidha Balozi wa Misri  hapa nchini Sherif Abdelhamid Ismail pamoja na mambo mengine ameahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwa pamoja na kuimarisha biashara na uwekezaji kwa ajili ya kunufaisha pande zote.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini Michael battle, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza  na Balozi wa Misri nchini Tanzania Sherif Abdelhamid Ismail (kushoto) pamoja na Ujumbe alioambatana nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages