Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam Edward Mpogolo, amewasisitizia viongozi wa kisiasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wa Serikali katika wilaya yake, kufanyakazi kwa kuzingatia mfumo wa kushirikiana kwa pamoja katika kujadili mipango ya maendeleo na changamoto za wananchi ili kufikia lengo linalokusudiwa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Amewataka pia kusimamia kwa pamoja kila mmoja kwa nafasi yake ya uongozi, mipango na miradi ya maendeleo kwa karibu ili kuleta matokeo chanya kwa kuwa kutofanya hivyo kunasababisha mipango na miradi hiyo kukwama na hivyo wananchi kubaki wakimlaumu mtendaji mkuu wa Serikali ambaye ni Rais.
DC Mpogolo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na viongozi wa CCM na wa Serikali kutoka Kata za Jimbo la Ukonga, akihitimisha ziara yake ya kujitambulisha kwao na kuwapa semina maalum ya kujenga uelewano wa kikazi kati yake na viongozi wa Chama na Serikali katika Wilaya yake.
Amehitimisha ziara hiyo akiwa ameshazungumza na viongozi wa kada hizo, katika Majimbo mengine yote yaliyomo katika Wilaya hiyo yakiwemo Ilala, Segerea ambako kila akipozungumza alisisitiza umuhimu wa viongozi wa Chama na serukali kushirikiana na kuwa karibu na shida za wananchi.
Amesema, ulazima wa viongozi hao kushirikiana upo kwa sababu, wa CCM na yule wa Serikali wote wajibu wao wa kwanza ni kushughulikia shida au changamoto za wananchi, na kimsingi zile shida zinazokuwa zinashughulikiwa na kiongozi wa CCM na zinazoshughulikiwa na yule wa Serikali zote ni za aina moja.
DC Mpogolo, alisema, katika ushirikiano huo, kiongozi wa Serikali hapaswi kudhani kuwa shughuli zinazofanywa na kiongozi wa Chama kuhudumia wananchi hazimhusu au yule wa Chama kudhani shughuli zinazofanywa na kiongozi wa serikali hazimhusu.
"Nataka niwaambieni, uhusiano ulipo katika ya Serikali Kuu na hizi za chini na wananchi ni kwamba msingi wa uhusiano huu ni Wananchi, maana hakuna kiongozi ambaye anapatikana bila maamuzi ya mwananchi.
Tazama, ili Chama kishike dola, kinaingia katika Uchaguzi, katika uchaguzi huo watu ndiyo wanakipa ridhaa ya kukifanya kiunde Serikali, sasa Chama kikishaunda Serikali maana yake ni kwamba wewe kiongozi wa Serikali usingepatikana kama Wananchi wasingechangua Chama.
Kwa hiyo hapo maana yake ni kwamba hakuna kiongozi wa Serikali ambaye ataacha kujali shida za watu wakati ametokana na Chama ambacho kimepewa nafasi na watu, na hata kwa mujibu wa Katiba Wananchi ndiyo msingi wa Mamlaka", akasema DC Mpogolo.
"Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana ukiwemo mkutano wa Chama wa kikatiba, anakuwemo wanashirikishwa viongozi wa kiserikali katika ngazi husika ambao wanatambuliwa na vikao husika kikatiba ya Chama, na vilevile katika Vikao vya Kiuongozi wa Serikali wapo viongozi wa Chama ambao hushiriki kwa mujibu wa katiba ya Chama.
Na utaratibu huu unafanyika kwa sababu ya kutaka Viongozi wa Serikali na wa Chama wapate fursa ya kujadili kwa pamoja changamoto zinazowakabili wananchi, kwa kuwa wanapozijadili kwa pamoja ndiyo ufumbuzi unapatikana", akasema DC Mpogolo.
Akasema, kwa hiyo ili viongozi washiriki vema katika vikao hivyo mtambuka ni lazima kila kiongozi kwa pande zote, kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika vikao vinavyohusu upande wake kujadili changamoto za wananchi, asipofanya hivyo maana yake akienda kwenye vikao mtambuka atakuwa hana ajenda zinazohusu wananchi badi ataenda na ajenda zake.
Unakuta kiongozi fulani wa Chama, mkewe amenyang'awa eneo la biashara na kiongozi wa Serikali pengine kwa mujibu a sheria, sasa kwa kuwa kiongozi huyo wa Chama hashiriki vikao vya Chama vinavyomhusu, akienda kwenye vikao mtambuka anaingia na ajenda ya mkewe kunyang'anywa eneo la biashara, wakati hiyo siyo ajenda ya wananchi.
"Sasa hali hii ya kukiuka mfumo ikiendelea inaleta matokeo mabaya hadi kwenye ngazi za juu za maamuzi, maana ngazi hiyo ya juu, inakuwa imefikishiwa ajenda ambazo si za wananchi, kwa hiyo matokeo yake miradi inakwama, wananchi wapati maendeleo, na kubaki wanamlaumu mtendaji wa mwisho, yaani rais wa Nchi kwa hafai.
Kwa hiyo tafadhalini sana, fanyeni kazi kwa kushirikiana viongozi wote, tufanye kazi kwa mshikamano na alama ya mshikamano ni maendeleo ya wananchi, msipofuata mfumo huu mnaumiza wananchi", akasema DC Mpogolo.
Baadaye DC Mpogolo alitoa nafasi kwa Wawakilishi kutoka Benki ya CRDB na Takukuru kuzungumza na kisha wakapewa nafasi madiwanin na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo kueleza kero kwa niaba ya wananchi, ambapo akijibu alisema, atazifanyia kazi.Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam Edward Mpogolo, akizungumza na Watendaji wa Serikali na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ukonga, katika Semina aliyoiitisha kwa ajili ya kujitambulisha na kuongeza uelewa wa pamoja katika utendaji kazi, iliyofanyika katika jimbo hilo, leo. Kulia ni Katibu Tawala wa Ilala Charangwa Selemani na Kushoto ni Diwani Kata hiyo Moahamed Bendera.
Madiwani wa Kata ya Ukonga wakimlaki DC Mpogolo ukumbini.
Wajumbe wa kikao hicho wakilmaki DC Mpogolo ukumbini.
Wajumbe wakimlaki DC Mpogolo ukumbini.
Wajumbe wakiwa wameketi ukumbini kusubiri DC Mpogolo azungumze nao
![]() |
| Madiwani wa Kata ya Ukonga wakiwa wameketi ukumbini kusubiri DC Mpogolo azungumze. |
Maafisa Tarafa wakiwa kwenye Kikao hicho
Katibu Tawala wa Ilala Charangwa Selemani akitoa utambulisho na madhumuni ya Mkutano huo.
Mwakilishi wa Benki ya CRDB akitoa somo kwa washiriki kuhusu umuhimu wa kutumia benki kuhifadhi akiba ya fedha.
Mwakilishi wa benki ya NMB akieleza umuhimu wa watu kuhifadhi fedha Benki.
DC Mpogoloa akijitambulisha na kutoa mada kwa viongozi wa CCM na wa serikali katika kikao hicho.
DC Mpogolo akiendelea kutoa mada
Wajumbe wa mkutano huo wakimsikiliza DC Mpogolo
"Hawa viongozi wa Chama na wa Serikali katika maeneo yenu mnaowaona hapa, msidhani wapo peke yake, kila mnayemuona hapa ana watu nyuma yake, kwa hiyo mkimsema vibaya mnakuwa mmewasema wengi", akasema DC Mpogolo.
"Awe Kiongozi wa Serikali au wa CCM lazima ajue kwamba Mamlaka ya uongozo ni ya wananchi, hata Katiba hii ndivyo inavyosema. Hivyo lazima kila kiongozi ajali shida za huyo mwananchi", akasema DC Mpogolo.
Diwani wa Ukonga akisalimia.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ukonga akifunga kikao.
DC Mpogolo akiwaaga wajumbe baada ya kikao.
Wajumbe wakimuaga DC Mpogolo.
Wajumbe wakimuaga kwa furaha DC Mpogolo.
DC Mpogolo akiagana na wajumbe.
DC Mpogolo akipanda gari tayari kuondoka kwenda kwenye majukumu mengine baada ya kikao hicho.
Mgambo akipiga Saluti kumuaga DC Mpogolo.

























No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇